12. Busara inaashiria haja


47- Ni katika adabu mtu kuashiria haja yake. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakifanya Mitume na watu bora na mawalii waliowafuata.

48- Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ

“Na Ayyuub alipomwita Mola wake [akiomba]: “Hakika mimi imenigusa dhara, Nawe ndiye mbora zaidi wa kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu”. (21:83)

Aliashiria tu na hakuomba moja kwa moja. Hali kadhalika ndivyo alivyofanya Muusa wakati alipokuwa amekaa chini ya kivuli:

فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ

“Basi akawanyweshea, kisha akageuka kwenda kivulini, akasema: “Mola wangu! Hakika mimi ni mhitajia wa kheri Utakayoniteremshia.” (28:24)

Alikuwa ni mwenye njaa alipoashiria hivyo. Na Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiangalia mbinguni akiashiria maombi. Hapo ndipo akaambiwa:

قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ ۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا

“Hakika Tumeona unavyogeuzageuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia.” (02:144)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 45
  • Imechapishwa: 18/03/2017