155. Arobaini ni desturi ya ki-Fir´awn


Swali 155: Ni upi msingi wa ukumbusho wa jambo la arobaini? Je, kuna dalili juu ya usuniwaji wa kumbukumbu[1]?

Jibu:

1 – Msingi wake ni kwamba ni desturi ya ki-Fir´awn iliokuwa kwa mafir´awn kabla ya Uislamu. Kisha ikaenea kutoka kwao na ikafika kwa wengine. Ni Bid´ah na maovu yasiyokuwa na msingi katika Uislamu. Yanarudishwa nyuma na yale yaliyothibiti katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayezua katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo basi atarudishiwa mwenyewe.”[2]

2 – Kumbukumbu na kumsifu maiti kwa njia inayofanyika leo ambapo watu wanakusanyika kwa ajili ya jambo hilo na kuchupa mpaka katika kumsifu ni jambo lisilojuzu. Amepokea Ahmad, Ibn Maajah na ameisahihisha al-Haakim kupitia kwa ´Abdullaah bin Abiy Awfaa ambaye ameeleza:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumsifu maiti.”[3]

 Isitoshe mara nyingi wakati mtu anataja sifa za maiti hujifakhari na kufanya upya machungu na masikitiko.

Ama ikiwa ni kumsifu tu wakati anapotajwa, wakati limepitishwa jeneza lake au kumtambulisha kwa kutaja matendo yake matukufu na mfano wa hayo kwa kitu kinachofanana na kusifu kwa baadhi ya Maswahabah kwa kufariki mmoja wao au mwengineo ni jambo linalofaa. Imethibiti kwamba Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) alisema:

“Kuna jeneza lilipitishwa ambapo likasifiwa kheri. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Imewajibika.” Likapita jeneza lingine na likasemwa vibaya. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Imewajibika.” ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) akasema: “Ni kipi kimewajibika?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Huyu amemsifu kheri na hivyo ikamthubutikia Pepo na yule mwengine amemsifu uovu imemthubutikia Moto. Nyinyi ni mashahidi wa Allaah ardhini.”[4]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/398-400).

[2] al-Bukhaariy (2697) na Muslim (1718).

[3] Ahmad (18659) na Ibn Maajah (1592) na tamko ni lake.

[4] al-Bukhaariy (1367) na Muslim (949).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 114-115
  • Imechapishwa: 27/01/2022