20- Subira haipingani na mwanamke kujizuiliwa kutokamana na mapambo yote kwa kuonyesha huzuni juu ya kufa kwa mtoto wake au mtu mwengine muda wa kuwa hatozidisha siku tatu. Isipokuwa mume wake ambaye anatakiwa kuacha kujipamba mieiz mine na siku kumi. Hayo ni kutokana na Hadiyth ya Zaynab bint Abiy Salamah aliyesimulia:

“Niliingia nyumbani kwa Umm Habiybah, mkewe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye akasema: “Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho akaacha kujipamba kwa juu ya maiti zaidi ya siku tatu isipokuwa kwa mume wake (ataonyesha huzuni) miezi mine na siku kumi.” Kisha nikaingia nyumbani kwa Zaynab bint Jahsh – wakati alipofariki kaka yake ambapo akaagizia aletewe mafuta mazuri akajipamba kisha akasema: “Sikuwa mimi na haja ya mafuta mazuri isipokuwa tu nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:… akaelezea Hadiyth.”

Ameipokea al-Bukhaariy (03/114, 09/400-401).

21- Lakini akiendelea kujipamba kwa lengo la kumfurahisha mume na kumkidhia mahitajio yake basi ndio bora kwake. Nyuma ya hilo kunatarajiwa kheri nyingi kama ilivyotokea kwa Umm Sulaym na Abu Twalhah al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Hakuna neno nikihadithia kisa chao hapa juu ya hilo – pamoja na urefu wake – kutokana na ile faida, mawaidha na mazingatio yaliyomo ndani yake. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Maalik, Abu Anas, alisema kumwambia mke wake Umm Sulaym – ambaye ni mama yake Anas: “Hakika bwana huyu – akimaanisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaharamisha pombe – akaondoka mpaka akafika Shaam na akafilia huko. Abu Twalhah akaja na akamposa Umm Sulaym na akamzumgumzisha juu ya hilo. Umm Sulaym akasema: “Ee Abu Twalhah! Harudishwi mtu mfano wako. Lakini wewe ni mtu kafiri na mimi ni mwanamke muislamu sifai kuolewa na wewe.” Akasema: “Unakataa maisha yako.” Umm Sulaym: “Ni yepi hayo?” Akasema: “Vya njano na vyeupe.” Umm Sulaym akasema: “Mimi sitaki vya njano na vyeupe. Ninachotaka kutoka kwako ni Uislamu. [Ukiingia katika Uislamu basi hayo ndio mahari yangu na sintokuomba kitu kingine]. Akasema: “Nimuona mimi nani kwa hilo?” Umm Sulaym akasema: “Nenda kwa ajili hiyo kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Abu Twalhah akaenda kumtafuta Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekaa kati ya Maswahabah zake. Alipomuona akasema: “Amekujieni Abu Twalhah akiwa na nuru ya Uislamu usoni kati ya macho yake. Akamweleza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyosema Umm Sulaym ambapo akamuoa kutokana na hilo. Thaabit akasema: [Ambaye ni al-Bunaaniy mmoja katika wapokezi wa kisa kutoka kwa Anas] hatukufikiwa na khabari kwamba kulikuwa na mahari yaliyokuwa matukufu zaidi kushinda kuridhia kwake (Umm Sulaym) Uislamu. Akamuoa na (Umm Sulaym) alikuwa ni mwanamke mwenye macho mazuri yenye udogoudogo. Akawa naye mpaka akamzalia mtoto. Abu Twalhah alikuwa anampenda mapenzi makubwa. Mtoto yule akaugua [ugonjwa mkubwa] Abu Twalhah akanyongeka juu ya kuugua kwake au akawa na msongo mkubwa wa mawazo juu yake. [Akawa Abu Twalhah anasimama juu ya swalah ya Fajr akitawadha na akienda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akiswali pamoja naye na akikaa naye mpaka karibu na nusu ya mchana akirudi, akilala usingizi wa mchana na akila. Akiswali Dhuhr hujiandaa na kwenda zake na harudi mpaka wakati swalah ya ´Ishaa]. Abu Twalhah akaondoka mida ya jioni kwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). [Katika upokezi mwingine: “Kwenda msikitini]. Mtoto yule akafa. Umm Sulaym akasema: “Tafadhalini asitoe khabari za kifo kwa Abu Twalhah yeyote mpaka mimi ndiye nimweleze. Akamwandaa yule mtoto [akamfunika] na akamweka upande fulani [miongoni mwa pande za nyumba]. Abu Twalhah akaja kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka alipoingia nyumbani kwake Umm Sulaym akiwa [alikuwa na marafiki zake kutoka msikitini]. Akasema: “Mtoto wangu anaendeleaje?” Akasema: “Ee Abu Twalhah!  Tangu kuumwa kwake hajatulizana kama alivyotulizana hivi sasa [nataraji amepumzika]. Akamletea chakula chake cha usiku. [Akawasogezea kile chakula wakala kisha watu wale wakaondoka]. [Akainuka kwenda kitandani mwake na akaweka kichwa chake chini] kisha Umm Sulaym akaamka na akajipaka manukato [akajipura vizuri zaidi kuliko vile alivyokuwa akijipura kabla ya hapo]. [Kisha akaja na akalala kitandani pamoja naye. Hakuwa isipokuwa kuhisi harufu ya mafuta mazuri iliokuwa ikitokea kwake yale yanayomtokea mwanaume kwa mkewe]. [Ilipofika mwisho wa usiku] Umm Sulaym akasema: “Ee Abu Twalhah! Unaonaje endapo kuna watu wameazima kipawa kutoka kwa watu kisha wale walioazima wakawaomba ni sawa wakawakatalia?” Akasema: “Hapana.” Umm Sulaym akasema: “Hakika Allaah (´Azza wa Jall) alikuwa ametuazima yule mtoto wako kama vile kipawa kisha akamchukua. Hivyo taraji malipo kutoka kwa Allaah na fanya subira.” Akakasirika kisha akasema: “Hivi kweli umeniacha mpaka nimefanya niliyoyafanya na hukunijuza kuhusu mwanangu?” [Akasema: “Sisi ni wa Allaah na Kwake ndiko tutarejea na akamhimidi Allaah]. Wakati asubuhi ilipoingia akaoga] kisha akaamkia kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) [akaswali pamoja naye] na akamkhabarisha. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaah akubarikini kwa lile lilofanyika usiku wenu.” Akapatwa na ujauzito kutokana na hilo. Umm Sulaym alikuwa akisafiri pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); akitoka pindi anapotoka, akiingia pamoja naye pindi anapoingia. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Atakapojifungua basi nileteeni mtoto huyo.” [Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa katika safari akiwa pamoja naye (Umm Sulaym) na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapoingia al-Madiynah kutoka safarini basi haingii wakati wa usiku, wakakurubia al-Madiynah na akajiwa na uchugu wa uzazi na Abu Twalhah akazuilika naye. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaondoka. Abu Twalhah akasema: “Ee Mola wangu! Hakika Wewe unajua kuwa mimi napenda kutoka pamoja na Mtume Wako pindi anapotoka na kuingia naye (al-Madiynah) pindi anapoingia na nimezuilika na kile unachokiona. Mara Umm Sulaym akasema: “Ee Abu Twalhah! Sihisi tena kile nilichokuwa nahisi.” Wakaondoka na akajiliwa tena na uchungu pindi walipofika]. Akamzaa mtoto wa kiume. Akamwambia mtoto wake Anas: “Ee Anas! Asilishwe kitu mpaka asubuhi mapema uamkaye naye kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). [Akamwigizia pia vijitende]. Akalala usiku mzima akilia na nikakesha nikiwa hali ya kuwa nimemili kwake yeye ninamchunga mpaka kukapambazuka. Nikaenda asubuhi na mapema kwenda kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) [akiwa amejifunika shuka] ilihali ni mwenye kuwaweka alama ngamia au mbuzi [waliomfikia]. Alipomuona akasema kumwambia Anas: “Amejifungua binti wa Milhaan?” Akamjibu: “Ndio.” [Akasema: “Nisubirie kidogo naja kwako]. Akasema: “Akakitupa kilichokuwemo mikononi mwake na akampokea mtoto yule na akasema: [“Ana chochote?” Wakasema: “Ndio, vijitende]. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akachukua [baadhi ya] zile tende [akazitafunatafuna kisha akakusanya ule ute wake] [kisha akamfungua kinywa chake na kumtumbukizia ndani yake] na akamfanyia yule mtoto Tahniyk na yule mtoto akawa anaramba: [akawa anafyonza baadhi ya utamu wa tende na ute wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikawa kitu cha kwanza kilichofungua tumbo la yule mtoto ni ute wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akasema: “Tazama namna Answaar wanavyopenda tende. [Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Mpe jina. Akasema] [Akamfuta uso wake] akamwita “´Abdullaah”. [Hakukuweko katika Answaar kijana ambaye ni mbora zaidi kuliko yeye]. Wakatoka kutokamana na yeye wapambanaji wengi na  ´Abdullaah huyu aliuwawa shahidi huko Faaris].

Ameipokea at-Twayaalisiy (2056) na mtiririko ni wake na al-Bayhaqiy (04/65-66) kupitia njia yake, Ibn Hibbaan (725), Ahmad (03/105-106, 181, 196, 287, 290). Ziada zote ni zake, kama itavyokuja huko mbele.

Ameipokea vilevile al-Bukhaariy (03/132-133), Muslim (06/174-175) kwa ufupi kwa kuishilia juu ya kisa cha kufa kwa mtoto huyo. an-Nasaa´iy (02/87) amepokea kipande katika mwanzo wake, ziada za kwanza ni zake, ziada ya sita, ya nane na ya kumi na sita ni ya al-Bukhaariy, zida ya kumi na tisa na ya ishirini na mbili ni ya Muslim. Na nyenginezo ni za Ahmad, kama ilivyotangulia.

Nimetilia umuhimu maalum kwa kukusanya mapokezi ya kisa hiki na matamshi yake kutokana na uzuri na utukufu uliyomo ndani yake na ili msomaji aweze kupata fikira pevu na za kweli. Kwa hayo mazingatio na faida zinapata kukamilika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 33-38
  • Imechapishwa: 31/12/2019