15. Suurah “al-´Aswr” inatosha kuwa hoja juu ya viumbe

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Lau Allaah Asingeliteremsha hoja yoyote kwa viumbe Wake isipokuwa Suurah hii, basi ingeliwatosheleza.”

MAELEZO

Maelezo haya yanaonyesha ukina wa uelewa wa ash-Shaafi´iy na utambuzi wake wa maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Namna hii kila ambaye atatazama kwa makini ataona kuwa lau Allaah asingeliwateremshia viumbe Suurah nyingine zaidi ya Suurah hii ambayo ndani yake kuna kuwalingania viumbe kuamini kila ambacho ni lazima kukiamini. Kwa sababu Allaah amesema:

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا

“… isipokuwa wale walioamini.”

Ndani yake pia kuna kuita katika matendo mema kwa aina mbalimbali za ´ibaadah katika faradhi, zilizo za wajibu na zilizopendekezwa. Kadhalika ndani yake kuna kuwaita watu kuyatendea kazi na kuwa na uvumilivu juu ya maudhi yanayomkumba mtu.

Kwa hivyo ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) ana haki ya kusema kwamba lau asingeliteremsha hoja juu ya viumbe Wake isipokuwa Suurah hii ingewatosha. Tusemeje ilihali Allaah ameteremsha Aayah mia moja na kumi na nne? Zipo ambazo ni refu, za wastani na za chini ya hapo, kama inavyofahamika. Kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) ameteremsha Qur-aan hii na akajipa jukumu mwenyewe la kuihifadhi. Amesema:

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ

“Hakika Sisi Tumeteremsha Ukumbusho huu na hakika Sisi bila shaka ndio Tutakaouhifadhi.”[1]

[1] 15:09

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Twariyqal-Usuwl ilaa idhwaah-ith-Thalaat-il-Usuwl, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 24/11/2021