15. Ni yepi malengo ya al-Ikhwaan al-Muslimuun kumwingiza kila mtu katika safu zao?


Swali 15: Je, katika mtandao wa al-Ikhwaan al-Muslimuun kunaingia mapote ya Kiislamu kama mfano wa Raafidhwah, Suufiyyah, Mu´tazilah au [ni mtandao wa] Sunnah iliosafi?

Jibu: Wao wenyewe wanalitambua hilo. Baadhi ya wale ambao wametoka kati yao wanalitambua hilo. Hata Muhammad Suruur ambaye alikuwa pamoja nao makumi ya miaka anawakosoa katika hili na anasema yafuatayo:

“Kundi hili limekusanya Salafiy, Suufiy, Mu´taziliy na wengineo. Hakutarajiwi mafanikio kwa kundi kama hili.”

Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba hili ni jambo linalojulikana kwao. Viongozi wao wanalitambua. Hilo ni kutokana na kwamba wanasema kuwa watu wote hawa ni waislamu. Kuna malengo gani ya kukusanya makundi yote haya ambayo yanatofautiana katika mambo ya ´Aqiydah? Malengo ya al-Ikhwaan al-Muslimuun ni kuwa na idadi ya wafuasi wengi wakati wa kupiga kura serikalini. Wanacholenga ni kupata kura nyingi sawa ziwe zimetokamana na makundi au watu binafsi. Haya ndio malengo yao.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 16/07/2017