15. Ni nini maana ya kuamini siku ya Mwisho na imejumuisha nini?


Swali 15: Ni nini maana ya kuamini siku ya Mwisho na imejumuisha nini?

Jibu: Kila kilichotajwa katika Qur-aan na Sunnah katika mambo yatayopitika baada ya mauti. Yote haya yanaingia katika imani ya kuamini siku ya Mwisho.

Mfano wa hilo ni kama hali za ndani ya makaburi kama neema na adhabu zinazopatikana ndani yake.

Mfano wa hilo ni kama hali za siku ya Qiyaamah kama hesabu, thawabu, adhabu, kugawiwa madaftari, mizani na uombezi.

Mfano wa hilo ni Pepo na Moto, sifa zake, sifa za wakazi wake na yale yote Allaah aliyowaandalia [wakazi wake]. Yote hayo yanaingia katika imani ya kuamini siku ya Mwisho.