15- Madhambi yanamfanya yule mtenda dhambi kuyachukulia wepesi


Mtenda dhambi huendelea kufanya madhambi mpaka ikafikia akayachukulia wepesi na kuyadharau katika moyo wake. Hiyo ni alama ya maangamivu. Kila pale ambapo dhambi itadharauliwa machoni mwa mja inakuwa kubwa mbele ya Allaah. al-Bukhaariy amepokea katika “as-Swahiyh” yake kutoka kwa Ibn Mas´uud aliyesema:

“Muumini huyaona madhambi yake kama vile yuko chini ya mlima na anaogopa usije kumuangukia. Mtu muovu huyaona madhambi yake kama vile nzi inayodema puani mwake ambapo akaiwekea kidole iruke.”

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 70
  • Imechapishwa: 08/01/2018