15. Dalili ya kumi na tatu kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


13- Imaam na Faqiyh Najm-ud-Diyn Abul-´Abbaas Ahmad bin Muhammad bin Khalaf aliniandikia:

“Nimemuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usingizini ambapo nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nataka kukuuliza kitu.” Akasema: “Kipi?” Akasema: “Imekuja katika Qur-aan na Hadiyth Swahiyh ya kwamba Allaah yuko juu ya mbingu, lakini hata hivyo kuna watu wengi wanaopinga hilo.” Akasema: “Ni nani anayepinga? Allaah yuko juu ya mbingu.”

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 86
  • Imechapishwa: 02/06/2018