15. Dalili juu ya mkono wa Allaah

15- Abul-Fadhwl Ja´far bin Muhammad bin Ya´quub as-Sandaliy ametuhadithia: al-Hasan bin Muhammad as-Sabaah az-Za´faraaniy ametuhadithia: Shabaabah bin Sawwaar ametuhadithia: Warqaa´ ametuhadithia, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa al-A´raj, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkono wa kuume wa Allaah (´Azza wa Jall) umejaa. Haupungui kwa kutoa mchana na usiku. Mnaonaje yale aliyotoa tangu aumbe mbingu na ardhi pasi na kupungua chochote kilichoko katika mkono Wake wa kuume? ´Arshi Yake iko juu ya maji na kwenye mkono Wake mwingine kuna mzani ambao ndiyo anashusha na kupandisha.”[1]

[1] al-Bukhaariy (4684), Muslim (993), Ahmad (2/242) na at-Tirmidhiy (3045) aliyesema:

“Hadiyth hii ni nzuri na Swahiyh na ndio inayofasiri Aayah:

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ

“Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah imefumbwa”. Mikono yao ndio iliyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema. Bali mikono Yake imekunjuliwa hutoa atakavyo.” (05:64)

Hadiyth imepokelewa na maimamu. Tunaiamini kama ilivyonakiliwa bila ya maana wala kuifanyia namna. Hivyo ndivyo walivyosema maimamu wengi akiwemo Sufyaan ath-Thawriy, Maalik bin Anas, Ibn ´Uyaynah, Ibn ´Uyaynah na Ibn-ul-Mubaarak; zinatakiwa kusimuliwa na kuaminiwa bila kuzifanyia namna.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 05/11/2017