146. Wafiwa ndio wanatakiwa kupelekewa chakula

Swali 146: Ni ipi hukumu ikiwa chakula wanacholishwa wafiwa wa maiti ni kichinjwa[1]?

Jibu: Hapana neno. Wafanyiwe chakula hicho na majirani au ndugu jamaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamrisha familia yake kuwatengenezea familia ya Ja´far bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) chakula wakati alipofikiwa na khabari ya kifo chake kutoka Shaam ambapo akasema:

“Watengenezeeni familia ya Ja´far chakula. Kwani hakika wamefikwa na kitu kinachowashughulisha.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/386-387).

[2] Ahmad (1754), Ibn Maajah (1610), at-Tirmidhiy (998) na Abu Daawuud (3132).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 106-107
  • Imechapishwa: 22/01/2022