145. Dalili kwamba anayekufuru kufufuliwa anakufuru

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Yule mwenye kukanusha kufufuliwa anakufuru. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

”Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: “Bali hapana! Naapa kwa Mola wangu! Bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale yote mliyoyatenda, na hayo kwa Allaah ni mepesi.”[1]

MAELEZO

Yule mwenye kukanusha kufufuliwa anakufuru – Kwa sababu amepinga nguzo miongoni mwa nguzo za imani. Jengine ni kwa sababu amemkadhibisha Allaah, Mitume Yake na Vitabu Vyake. Kwa sababu Allaah ameeleza kuhusu kufufuliwa. Mitume wameeleza kuhusu kufufuliwa. Vitabu vimeeleza kuhusu kufufuliwa. Kwa hiyo yule mwenye kupinga amekufuru. Dalili ya hiyo ni maneno Yake (Ta´ala):

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا

”Waliokufuru wamedai… ”

Madai ni wongo.

أَن لَّن يُبْعَثُوا

”… kwamba hawatofufuliwa kamwe.”

Kwa hiyo Aayah imefahamisha kwamba kupinga kufufuliwa ni ukafiri. Wanasema kuwa hakuna kufufuliwa baada ya kufa. Washirikina na waabudu masanamu katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakibisha kuhusu kufufuliwa:

أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ

”Je, hata tukiwa ni mifupa iliyosagika na kuoza? Watasema: ”Basi marejeo hayo ni yenye khasara.”[2]

Walisema:

مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ

“Ni nani atakayehuisha mifupa hii ilihali imekwishaoza na kusagika na kuwa kama vumbi?”[3]

Moja katika ubishi wao walisema:

أَيَعِدُكُمْ أَنَّكُمْ إِذَا مِتُّمْ وَكُنتُمْ تُرَابًا وَعِظَامًا أَنَّكُم مُّخْرَجُونَ هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ

“Je, anakuahidini kwamba nyinyi mkifa, mkawa udongo na mifupa kwamba hakika mtatolewa? Hayawi kabisa, hayawi kabisa hayo mnayoahidiwa.”[4]

Yapo maneno mengine ya kikafiri kutoka katika nyumati zilizotangulia na kutoka kwa washirikina katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yule mwenye kukadhibisha kufufuliwa basi yeye yuko pamoja na hawa makafiri. Hakuna anayepinga kufufuliwa isipokuwa kafiri. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amemwamrisha Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aape kwa jina Lake juu ya kufufuliwa. Alisema:

قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي

”Sema: “Bali hapana! Naapa kwa Mola wangu! Bila shaka mtafufuliwa.”

Hili ni fungu:

لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ

”… mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale yote mliyoyatenda.”

Aayah hii ni moja katika Aayah tatu ambazo Allaah anamwamrisha Mtume Wake kuapa juu ya kufufuliwa:

Aayah ya kwanza: Katika Suurah ”Yaa Siyn”:

وَيَسْتَنبِئُونَكَ أَحَقٌّ هُوَ ۖ قُلْ إِي وَرَبِّي إِنَّهُ لَحَقٌّ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ

”Wanakuuliza: ”Je, hayo ni kweli?” Sema: ”Ndio, naapa kwa Mola wangu! Hakika hayo bila shaka ni kweli nanyi si wenye kushinda.”[5]

Aayah ya pili: Suurah Sabaa´:

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَأْتِينَا السَّاعَةُ ۖ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأْتِيَنَّكُمْ عَالِمِ الْغَيْبِ ۖ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ لِّيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ

”Na wale waliokufuru wakasema: ”Saa haitotufikia.” Sema: ”Bila shaka! Naapa kwa Mola wangu itakufikieni, mjuzi wa mambo yaliyofichikana; hakuna kinachofichikana Kwake ingawa chenye uzito wa chembe mbinguni wala ardhini na wala kidogo zaidi kuliko hicho na wala kikubwa zaidi isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha ili awalipe wale walioamini na wakatenda mema – basi hao watapata msamaha na riziki tukufu.”[6]

Allaah amemwamrisha Mtume Wake kuapa juu ya kufufuliwa na juu ya Qiyaamah.

Aayah ya tatu: Ni ile ambayo tunaidurusu katika Suurah ”at-Taghaabuun”:

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

”Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: “Bali hapana! Naapa kwa Mola wangu! Bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale yote mliyoyatenda, na hayo kwa Allaah ni mepesi.”

Hekima ya kufufuliwa ni kuwalipa waja juu ya matendo yao. Maneno Yake (Ta´ala):

لَتُنَبَّؤُنَّ

”… mtajulishwa… ”

Bi maana mjuzwe matendo yenu na mlipwe kwayo.

[1] 64:07

[2] 79:11-12

[3] 36:78

[4] 23:35-36

[5] 10:53

[6] 34:03-04

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 284-286
  • Imechapishwa: 18/02/2021