144. Ibn Baaz kuhusu kukaa siku tatu nyumbani kwa mfiwa

Swali 144: Baadhi ya familia ya maiti wanakaa siku tatu. Ni ipi hukumu ya hilo[1]?

Jibu: Wakikaa ili watu waweze kuwapa mkono wa pole hakuna vibaya – Allaah akitaka – ili wasiwachoshe watu. Lakini wafanye hivo pasi na kuwatengenezea watu chakula.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/382).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 104
  • Imechapishwa: 22/01/2022