Swali 142: Je, kuna masiku yaliowekewa kikomo kwa ajili ya kutoa rambirambi? Kwa sababu inasemekana kwamba ni siku tatu peke yake[1].

Jibu: Hakuna siku zilizowekewa mpaka kwa ajili ya kutoa mkono wa pole. Bali imesuniwa kuanzia pale inapotolewa roho kabla ya kumswalia maiti na baada yake. Mwisho wake hauna kikomo katika Shari´ah takasifu. Ni mamoja hayo yamefanyika usiku au mchana. Ni mamoja hayo yamefanyika katika nyumba, barabara, msikitini, makaburini au maeneo mengine.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/379).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 21/01/2022