14. Uombaji wa kupanga


60- Ikiwa muombaji ni mkweli na ni mwenye kuhitajia ili kuweza kutatua haja na ufakiri wake, anaweza kuomba. Katika hali hii ni wajibu kwa waislamu kumpa, kama jinsi inavyotolea dalili Hadiyth ya mlango huu[1].

61- Ama ikiwa muombaji ni mng´ang´anizi na anachotaka ni kukuza pato lake ni ni katika wale ambao wamefanya kuomba ni mazowea na ndio kazi, apambanwe na kutimuliwa.

62- Ni kutokana na uombaji huu wa mwisho uliotajwa Maalik alionyesha machukizo yake dhidi yake. Kadhalika inahusiana na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) na Allaah ndiye anajua zaidi.

63- Mu´aadh bin Jabal amesema:

“Itapofika siku ya Qiyaamah atanadi mwenye kunadi: “Wako wapi wale watu wanaochukiwa na Allaah zaidi katika ardhi?” Tahamaki wajitokeze waombajiombaji kutoka misikitini.”

64- Abu Nadhwrah al-´Abdiy amesema:

“Nilikutana na wakati ambapo hakukuwepo na muombaji hata mmoja katika ardhi mbali na mtumwa ambaye anataka kujiachia huru na mwenye deni.”

[1] Bi maana mlango uliotangulia wa 13

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 49
  • Imechapishwa: 18/03/2017