137. al-Qummiy upotoshaji wake wa pili wa al-A´raaf

al-Qummiy amesema:

“Kuhusiana na maneno Yake:

إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ

“Hakika wale waliozikadhibisha Aayah Zetu na wakazifanyia kiburi, hawatofunguliwa milango ya mbingu na wala hawatoingia Peponi mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano – hivyo ndivyo Tunavyowalipa wahalifu.”[1]

baba yangu amenihadithia, kutoka kwa Fadhwaalah, kutoka kwa Abaan bin ´Uthmaan, kutoka kwa Dhurays, kutoka kwa Abu Ja´far aliyesema: “Aayah hii iliteremshwa kuhusu Twalhah, az-Zubayr na wale wengine wote walioshiriki vita vya ngamia.”[2]

Allaah amemtakasa Abu Ja´far kutokamana na uongo huu na kumzulia Allaah na Kitabu Chake.

Kwanza Aayah imeteremshwa wakati wa kipindi cha Makkah.

Pili inawazungumzia makafiri ambao walizikadhibisha Aayah za Allaah na wakawafanyia kiburi Mitume.

Tatu ni kwamba kuipachika kwa Twalhah na kwa az-Zubayr (ambao ni miongoni mwa wale vigogo wa Maswahabah na ni miongoni vilevile mwa wale kumi waliobashiriwa Pepo katika wale waliotangulia mwanzoni) ni dalili tosha juu ya chuki ya Baatwiniyyah ya kiajemi dhidi ya Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali ni chuki juu ya Uislamu na Mtume wa Uislamu. Hakuna mwenye kusema kwamba Pepo ni ya Raafidhwah Baatwiniyyah na Moto ni wa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa tu wale ambao ni waovu kabisa na uadui mkubwa dhidi ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 07:40

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/230).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 196-197
  • Imechapishwa: 31/08/2018