136. Kuwapokea wanaokuja kutoa pole


Swali 136: Ni yepi maoni yako juu ya mtu ambaye anaketi nyumbani kwa ajili ya kuwapokea wanaokuja kutoa pole pamoja na kuzingatia kwamba wengi katika wanaokuja kutoa pole hawawezi kufanya hivo isipokuwa nyumbani[1]?

Jibu: Sijui ubaya wowote kwa haki ya wale waliofikwa na msiba kwa kufariki kwa jamaa zao; mke wake na wengineo kuwapokea wanaokuja kutoa rambirambi nyumbani kwake katika wakati ambao ni wenye kufaa. Kutoa pole ni Sunnah. Kuwapokea wanaokuja kutoa pole ni miongoni mwa mambo yanayowasaidia kutekeleza Sunnah. Akiwakirimu kwa kahawa, chai au manukato yote hayo ni mazuri.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/373).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 99
  • Imechapishwa: 19/01/2022