132. Kumhukumu kifo ambaye ubongo wake umekufa


Swali 132: Madai ya madaktari – Allaah akuhifadhi – ni kwamba ambaye ubongo wake umekufa hauwezi kurudia uhai wake[1]?

Jibu: Madai haya si yenye kutegemewa wala hayatakiwi kufanyiwa kazi. Usahihi wake hauna dalili. Nimefikiwa na khabari kwamba wako baadhi ya wale ambao wameambiwa kuwa ubongo wao umekufa uhai wao ulirudi na wakaishi. Kwa hali yoyote kufa kwa ubongo hakuzingatiwi na wala mwenye hali hiyo hatohukumiwa hukumu ya kifo mpaka kihakikiwe kifo chake kwa njia isiyokuwa na shaka yoyote.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/366-367).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 95-96
  • Imechapishwa: 17/01/2022