13. Tofauti za Maswahabah hazikuwa kama tofauti za watu wa leo

Shubuha ya pili: Ikiwa kutofautiana katika dini ni jambo lililokatazwa. Unasemaje kuhusu kutofautiana kwa Maswahabah na maimamu baada yao? Je, kuna tofauti yoyote kati ya kutofautiana kwao na kutofautiana kwa wengine waliokuja baada yao?

Ndio. Kuna tofauti kubwa kwa sababu ya mambo mawili:

1- Sababu yake.

2- Athari yake.

Kutofautiana kwa Maswahabah ilikuwa ni jambo lisiloepukika na la kimaumbile kutokana na uelewa. Si kwamba wao wenyewe ndio walikuwa wanataka kutofautiana. Vilevile kulikuwepo mambo mengine katika zama zao yaliyopelekea katika tofauti na hivyo baadaye yakaondoka[1]. Mfano wa tofauti kama hii ni jambo haliwezi kumalizika kabisa kabisa. Wala wale wenye kufanya hivi hawaguswi na usemwaji vibaya uliotajwa katika Aayah zilizotangulia. Kwa sababu hawakukusudia wala kuliendelea.

Ama kuhusu tofauti za wale wenye kufuata kichwa mchunga, mara nyingi ni kwamba hawana udhuru wowote. Baadhi yao wanapobainikiwa kwamba madhehebu mengine yamejenga maoni yake juu ya dalili katika Qur-aan na Sunnah, wanayaacha kwa sababu tu maoni yake yanaonelea kinyume. Ni kama kwamba madhehebu yake ndio msingi na dini aliyoifikisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hayo madhehebu mengine ni dini nyingine iliyofutwa.

[1] Rejea katika kitabu ”al-Ihkaam fiy Usuul-il-Ahkaam” cha Ibn Hazm na ”Hujjatullaah al-Baalighah” cha ad-Dahlawiy na khaswakhaswa kitabu chake ”´Aqd-ul-Jayyid fiy Ahkaam-il-Ijtihaad wat-Taqliyd”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 53-54
  • Imechapishwa: 21/01/2019