Baadhi ya watu wanatumia hoja juu ya uzuri wa Bid´ah zao walizozua katika dini ya Allaah – Bid´ah ambazo zinapelekea katika mambo ambayo tumetangulia kuyataja kwa waliyoyazua kutokana na njia za malengo mazuri – juu ya ukusanywaji wa Qur-aan kwenye msahafu mmoja, kujengwa masomo ya kisasa na mengineyo ambayo ni njia tu na sio malengo. Kuna tofauti kati ya kitu ambacho ni njia inayopelekea kwenye malengo yenye kusifiwa yaliyothibitishwa katika Shari´ah lakini hata hivyo hayawezi kuhakikishwa isipokuwa mpaka zifanywe njia hizi. Njia hizi zinakuja mpyampya kwa kutegemea na wakati na zinatofautiana kwa kutofautiana kwa zama. Amesema (´Azza wa Jall):

وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ

“Waandalieni nguvu zozote mziwezazo.”[1]

Maandalizi ya nguvu yaliyokusudiwa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sio maandalizi ya nguvu katika zama zetu hizi. Midhali hatujazua kitendo ambacho kitatufanya kufikia kufanya maandalizi ya nguvu, basi uzushi huu ni wa njia na sio uzushi wa malengo anayojikurubisha nao mbele ya Allaah. Ni uzushi wa njia.

Miongoni mwa kanuni zilizothibitishwa na wanachuoni ni kwamba njia zina hukumu moja sawa na malengo. Kutokana na haya tunapata kujua kwamba yale wanayobwabwaja wazushi wanaozua katika dini ya Allaah kwa kutumia dalili kwa mfano wa mambo kama haya ya kwamba hawana kabisa ndani yake mategemezi. Inahusiana na njia zinazopelekea katika lengo lililosifiwa. Ukusanywaji wa Qur-aan kwenye vitabu na mfano wa hayo yote hayo ni njia zinazopelekea kwenye malengo yaliyowekwa katika Shari´ah.

Ni lazima kwa mtu kutofautisha kati ya malengo na njia. Yaliyokusudiwa kwa dhati yake umekamilika usuniwaji wake kupitia kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa yale ambayo Allaah amemteremshia kutoka kwenye Qur-aan na Sunnah twaharifu.

[1] 08:60

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 25/07/2019