Swali 13: Je, yule mwenye kujiita “Salafiy” anazingatiwa amejiweka kichama?

Jibu: Hakuna kosa lolote kujinasibisha na Salafiyyah[1] ikiwa kama ni hakika. Hata hivyo haijuzu kwake kujinasibisha na Salafiyyah ikiwa kama anadai tu hilo na yeye anafuata mfumo mwingine usiyokuwa mfumo wa Salaf. Kwa mfano Ashaa´irah wanasema kuwa ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Si sahihi kwa sababu fikira zao sio mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Vivyo hivyo Mu´tazilah wanajiita “Muwahhiduun”, wapwekeshaji.

Kila mmoja anadai kuwa yuko karibu na Laylaa

lakini Laylaa hawakubalii lolote katika hayo

Yule mwenye kudai kuwa anafuata mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah anatakiwa kufuata nyayo za Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na kuwaacha wanaoenda kinyume. Methali inasema kuwa haiwezekani kukusanya mjusi na nyangumi, bi maana wanyama wa jangwani na wanyama wa baharini. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawawezi kujumuishwa na wahalifu kama vile Khawaarij, Mu´tazilah na Hizbiyyuun ambao ni pamoja na wanaoitwa “waislamu wa sasa” ambao wanataka kujumuisha upotevu wa leo na mfumo wa Salaf. Hautofaulu mwisho wa ummah huu isipokuwa kwa yale yaliyowafanya wa mwanzo wao kufaulu. Kwa kifupi ni kwamba ni lazima kupambanua na kusafisha mambo.

[1] Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

“Hakuna aibu kwa yule mwenye kudhihirisha madhehebu ya Salaf, akajinasibisha nayo na akajitukuza kwayo. Bali ni wajibu kumkubalia hilo kwa makubaliano kwa sababu madhehebu ya Salaf si jengine isipokuwa ni haki” (Majmuu´-ul-Fataawaa (04/149))

Zingatia maneno ya Shaykh-ul-Islaam ambayo aliyazungumza miaka 800 ya nyuma. Kana kwamba anamraddi bwana mmoja anayeishi hii leo na anayejinasibisha na elimu. Mtu huyo amesema:

“Yule mwenye kumuwajibishia mtu mwingine kuwa Ikhwaaniy, Salafiy, Tabliyghiy au Suruuriy anatakiwa kuambiwa atubie. Akitubia ni sawa na vinginevyo auliwe.”

Ameyasema katika kanda ulioenezwa kwa vijana ulio na kichwa cha khabari “Firr min al-Hiziyyah Firaarak min al-Asad”.

Ametakasika Allaah kutokana na mapungufu! Ni vipi anaweza kujijuzishia yeye mwenyewe kutaja mfumo wa Salaf wa haki pamoja na mifumo na mapote haya yaliyozushwa na ya kipotofu? Swali langu kwa mtu huyu anayeishi katika nchi ya Tawhiyd na amechukua cheti cha pili katika Hadiyth na hivi karibuni amepata cheti cha udaktari: Awe kitu gani kama si Salafiy? ´Allaamah Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) aliulizwa:

“Unasemaje kuhusiana na mwenye kujiita “Salafiy” au “Athariy”? Je, ni kujitakasa?

Akajibu (Rahimahu Allaah):

“Haina neno ikiwa kama kweli ni Athariy au Salafiy. Kama ambavo baadhi ya Salaf walikuwa wakisema fulani ni “Salafiy” na “Athariy”. Kujitakasa kwa lazima. Kujitakasa kwa lazima.” (Kutoka katika kanda “Haqq-ul-Muslim” 1413/01/16 Twaaif)

Shaykh Bakr Abu Zayd amesema:

“Inaposemwa Salaf, Salafiyuun au mfumo wao ambao ni Salafiyyah, inahusiana na kujinasibisha kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na wale wote waliowafuata kwa wema pasi na yule aliyepinda katika matamanio yake… Wale walioshikamana imara na mfumo wa kinabii ananasibishwa na watangu wake wema katika hilo. Ndio maana wanaitwa “Salaf” na “Salafiyyuun”. Yule mwenye kujinasibisha na wao anaitwa “Salafiy”. Kutokana na hilo neno Salaf ni wale wema waliotangulia. Msemo huu unajumuisha kila yule mwenye kuwaiga Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ikiwa  ni pamoja na watu wa zama zetu, hivyo ndivyo wanavosema wanazuoni. Sio unasibishaji wa mielekeo inayoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Sio unasibishaji ambao kwa wakati hata mmoja umeenda kinyume na karne za kwanza; bali umetoka kwao na pamoja nao. Licha ya hivyo mtu hawezi kusema hivo kwa wale walioenda kinyume nao kwa jina au mwelekeo hata kama wataishi kati yao na wao.” (Hukm-ul-Intimaa´, uk. 46)

Amesema vilevile:

“Kuwa Salafiy katika njia iliyonyooka.” (Hilyatu Twaalib-il-´Ilm, uk. 08)

Unasibishaji huu umetajwa katika vitabu vya historia na vya wasifu. Imaam adh-Dhahabiy amesema kuhusu Muhammad bin Muhammad al-Bahraaniy:

“Alikuwa ni mtu wa dini, mwema na Salafiy.” (Mu´jam-ush-Shuyuukh (02/280))

Amesema kuhusu Ahmad bin Ahmad bin Ni´mah al-Maqdisiy:

“Alikuwa ni mwenye kushikamana na ´Aqiydah ya Salaf.” (Mu´jam-ush-Shuyuukh (01/34))

Kujinasibisha na Salaf ni jambo la lazima ili mtu Salafiy aweze kujitofautisha na yule mwenye kujificha na ili kila yule asiyetaka kujinasibisha na wao na kufuata mfumo wao aweze kutumbukia kwenye utatizi. Pindi mielekeo iliyopinda inakuwa mingi na vyama vya mapote potevu na vyenye kupotosha vinajitokeza, basi Ahl-ul-Haqq wanajinasibisha waziwazi na Salaf ili kujitenga mbali na wale wenye kwenda kinyume. Allaah (Ta´ala) amesema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waumini:

فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ

“Wakikengeuka, basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni waislamu.”” (03:64)

وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّـهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ

“Na nani mwenye neno nzuri zaidi kuliko yule anayelingania katika kumwamini Allaah, akatenda mema na akasema: “Hakika mimi ni miongoni mwa waislamu.”” (41:33)

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ

“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi – mimi na anayenifuata. Utakasifu ni wa Allaah na mimi si miongoni mwa washirikina.” (12:108)

Baada ya kumaliza kuandika kitabu hichi nilipata karatasi mbili tatu ambapo ´Aa´idh al-Qarniy alijirudi katika baadhi ya makosa yake ikiwa ni pamoja na hili. Ili niwe mwadilifu na kutokuwa mwenye kupendelea naamua kutaja ya kwamba amejirudi katika hilo pamoja na kwamba kuna baadhi ya mambo ya namna ya kujirudi kwake na usulubu ambayo yanatakiwa kukumbushwa na inaitwa kutelekezwa. Anasema:

“Kumi na nne: Katika kanda “Firr min al-Hizbiyyah Firaarak min al-Asad” nimesema: “Yule mwenye kumuwajibishia mtu mwingine kuwa Ikhwaaniy, Salafiy, Tabliyghiy au Suruuriy anatakiwa kuambiwa atubie. Akitubia ni sawa na vinginevyo auliwe.” Nimesema makosa na ninamuomba Allaah msamaha. Nimemaanisha yule mwenye kusema hivo ametunga Shari´ah. Hata hivyo ni makosa kwa hali yoyote na ninaomba udhuru kwa hilo. Ninaonelea kuwa mfumo wa Salaf ndio wa haki ambao ni wajibu kwa watu kuufuata na kuuchukua.”

Ni jambo lenye kujulikana kutoka katika madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ya kwamba makosa yote yanatakiwa kujirudi na si kutubia tu. Kukubali, kusahihisha na kujirudi yanatakiwa kuandikwa waziwazi na hadharani ili watu wote wapate kujua hilo – na si kwenye karatasi mbili tatu tu ambazo hakuna wenye kuzijua isipokuwa wachache mno. Hebu wacha msomaji ajionee ujinga huu! Ibn-ul-Qayyim amesema:

“Moja miongoni mwa masharti ya mlinganizi katika Bid´ah kutubu ni kwamba abainishe kuwa alikuwa akilingania katika Bid´ah na upotevu na kinyume chake ndio sahihi.” (Uddat-us-Swaabiriyn, uk. 93)

Halafu isitoshe jengine ninalouliza ni kama ilikuwa kosa moja tu ambalo mlinganizi huyu ambaye hivi karibuni amechukua udaktari wake alilofanya. Anasema katika kitabu chake “al-Misk wal-´Anbar”:

“Ni maonyesho yepi tuliyofanya mwaka uliyopita? Unaweza kujiuliza na mimi. Ni jambo la kujiuliza jinsi wanavyoshikamana na kuhajiri kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yako wapi magazeti ya asubuhi? TV? Ni kwa nini magazeti hayasherehekei Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Hakuna nchi yoyote isipokuwa watu wanamtambua, lakini pamoja na hivyo hawamsherehekei. Hata neno moja? Hata msitari mdogo tu? Hata ibara ndogo tu yenye kusherehekea muhuishaji huyu mkubwa? (01/189)

Hili si linafanana, hata kama sio sawasawa kabisa, na sherehe ya maulidi iliyozushwa inayosherehekewa kwenye vyombo vyote vya khabari mbali na nchi hii ya ki-Sunniy Salafiy, Saudi Arabia. Mlinganizi huyu akakazia msimamo wake uliopetuka mipaka katika kusherehekea kuhajiri kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuuliza:

“Vipi watajipa udhuru kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hiyo kesho?” (01/190)

Anakusudia vyombo vya khabari ambavyo havikusherehekea Hijrah na kuonyesha hilo. Kabla ya hapo alipetuka mipaka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema:

“Ama kuhusiana na mkombozi wa kwanza, kiumbe aliye mwenyewe na mtu ambaye Allaah ameunyoosha ummah kwake, hakuna mawaidha wala wasifu.”

Hili si jengine isipokuwa madhehebu ya Suufiyyah. Ni vipi mlinganizi anaweza kuutuhumu ummah ya kwamba haukuandika wasifu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Kwa njia hiyo anawatuhumu Salaf wetu. Ni vitabu vingapi vilivyoandika historia na sifa zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)! Na ikiwa anakusudia kuwa kuhajiri kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutajwe kwa njia kama ya usherekeaji wa maulidi, ninamuomba Allaah atulinde. Khabari zaidi soma katika ukurasa wa 253 ili uone aliyosema baada ya kuwa sugu kwa miaka kumi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 35-39
  • Imechapishwa: 11/06/2017