13. Msingi wa nne: Kutilia umuhimu ´Aqiydah ya Salaf

4- Kutilia umuhimu ´Aqiydah ya Salaf kwa kuisoma, kimatendo na kuifunza

Miongoni mwa mambo yanayositikisha ni kwamba kipindi cha mwisho tumekuwa ni wenye kusikia maneno yanayoitupilia mbali ´Aqiydah na kuitenga mbali na uwanja wa yale mambo yanayotiliwa umuhimu. Yako makundi ambayo yanazingatiwa mambo ya ´Aqiydah ni miongoni mwa ya kisehemusehemu ambayo hayatiliwi umuhimu. Bali wako wanaosema kuwa hakuna kinachowadhuru endapo watamthibitishia au kutomthibitishia Allaah mkono. Haya ni miongoni mwa majanga. Ni jambo linalojulikana kwa kila mtu namna ambavo ´Aqiydah na Tawhiyd vina nafasi ya juu katika Shari´ah. Viumbe wameumbwa kwa lengo kuu ambalo ni kumwabudu Allaah (Ta´ala). Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

”Na Sikuumba majini na watu wa isipokuwa waniabudu.”[1]

Allaah hakuwatumiliza Mitume wala hakuteremsha vitabu isipokuwa ni kwa sababu ya kuhakikisha Tawhiyd na kuwalingania watu katika jambo hilo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ بِالرُّوحِ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ أَنْ أَنذِرُوا أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاتَّقُونِ

“Anateremsha Malaika kwa Roho kwa amri Yake juu ya amtakaye miongoni mwa waja Wake kwamba: “Onyeni ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Mimi, hivyo basi nicheni.”[2]

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mungu wa haki isipokuwa Mimi; hivyo basi niabuduni.”[3]

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

”Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut [waungu batili].”[4]

Amri ya kwanza ndani ya Qur-aan tukufu ni maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kumcha.”[5]

Kitu cha kwanza Mitume walichokuwa wakianza kuwalingania watu wao ilikuwa:

يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ

“Enyi watu wangu! Mwabuduni Allaah, kwani hamna mungu wa haki mwingine asiyekuwa Yeye.”[6]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliishi miaka ishirini na tatu akilingania kwa Allaah. Katika miaka hiyo miaka kumi na tatu alikuwa Makkah na kumi katika hiyo alikuwa akithibitisha Tawhiyd, akilingania kwayo, akipambana na shirki, akitahadharisha nayo na sehemu ya maisha yake iliyobaki (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akithibitisha na kusimika Tawhiyd na akibainisha hukumu mbalimbali za dini. Yote haya yanaonesha dalili ya wazi juu ya kutilia umuhimu mambo ya ´Aqiydah kwa kujifunza na kuyafunza, akiyatendea kazi na kuyalingania.

Yote hayo ni kwa sababu Tawhiyd ikisalimikaa kutokamana na uchafu basi si vyengine isipokuwa mwenye nayo ataingia Peponi. Haijalishi kitu hata kama ni mtenda madhambi makubwa. Watenda madhambi makubwa wako chini ya utashi wa Allaah; akitaka ataanza kuwaadhibu kwanza kisha baadaye awaingize Peponi kwa sababu ya Tawhiyd yao, na kabla ya hilo kwa sababu ya fahdilah na ukarimu Wake (Subhaanah), na Allaah akitaka atawasamehe.

Unakaribia kutompata yeyote ambaye ´Aqiydah yake imesalimika isipokuwa utaona matendo mema na mambo mengine ya utiifu yanakuwa mepesi kwake. Kwa ajili hiyo kuitilia umuhimu ´Aqiydah na kuirekebisha ikawa ni miongoni mwa matendo matukufu na makubwa zaidi.

[1] 51:52

[2] 16:02

[3] 21:25

[4] 16:36

[5] 02:21

[6] 07:59

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 41-43
  • Imechapishwa: 06/08/2020