13. Hadiyth “Yule atakayesimama usiku wa makadirio kwa imani na kwa matarajio… “


1104- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesimama usiku wa makadirio kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa yale madhambi yake yaliyotangulia. Yule atakayefunga Ramadhaan kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa yale madhambi yake yaliyotangulia.”[1]

Katika upokezi wa Muslim imekuja:

“Atakayesimama usiku wa makadirio na akauafiki – na nadhani amesema “kwa imani na kwa matarajio” – basi atasamehewa yale madhambi yake yaliyotangulia.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/587)
  • Imechapishwa: 26/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy