13. Hadiyth “Kitu bora ambacho mtu anaweza kukiacha baada ya kutoweka… “


79- Abu Qataadah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kitu bora ambacho mtu anaweza kukiacha baada ya kutoweka ni mambo matatu;  mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa, swadaqah yenye kuendelea ambayo analipwa kwayo na elimu inayotendewa kazi baada yake.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/143)
  • Imechapishwa: 24/09/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy