13. Daktari wa kiume kukaa chumba kimoja na muuguzi au daktari wa kike

Swali 13: Mimi ni daktari wa kiume kwenye chumba cha uchunguzi nakuwa na muuguzi wa kike kwenye chumba hichohicho. Kiasi cha kutujia mgonjwa tunakuwa tumeshaongea mambo mbalimbali. Shari´ah inasemaje juu ya jambo hili?

Jibu: Hukumu ya jambo hili ni kama hukumu ya kabla yake[1]. Haijuzu kwako kukaa faragha na mwanamke. Haijuzu kwa muuguzi wa kiume au daktari wa kiume kukaa chemba na muuguzi wa kike au daktari wa kike. Ni mamoja katika chumba cha uchunguzi wala kwenginepo kutokana na Hadiyth tuliotangulia kutaja. Jambo hilo linapelekea katika fitina isipokuwa yule aliyerehemewa na Allaah. Ni lazima wanaume wafanyiwe uchunguzi na wanaume peke yao na wanawake wafanyiwe uchunguzi wa wanawake peke yao.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/12-wafanyakazi-wa-mahospitali-mwanaume-kukaa-faragha-na-mwanamke/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 35
  • Imechapishwa: 06/07/2019