124. Aina ya nne ya waislamu kuwafanya makafiri marafiki na vipenzi

4- Fungu la nne: Ni yule mwenye kuwasaidia makafiri dhidi ya makafiri ambao wana mkataba na waislamu, kitendo hichi ni haramu na wala haijuzu, kwa sababu waislamu watakuwa wamevunja mkataba. Makafiri wenye mkataba na waislamu haijuzu kwa muislamu yeyote yule kuwapiga vita. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule atakayemuua [kafiri] mwenye mkataba [na waislamu], basi hatonusa harufu ya Pepo.”[1]

Ikiwa Allaah (´Azza wa Jall) amewakataza waislamu kuwasaida waislamu wenzao dhidi ya makafiri wenye mkataba kwa waislamu, tusemeje kuhusu yule mwenye kuwasaidia makafiri katika kuvunja ahadi ya waislamu? Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ إِلَّا عَلَىٰ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ

“Wakikuombeni msaada kwenu katika dini, basi ni juu yenu kuwasaidia – isipokuwa juu ya watu mliofungamana mapatano kati yenu na wao.” (al-Anfaal 08:82)

Waislamu wakituomba msaada dhidi ya makafiri basi ni lazima kwetu kuwasaidia waislamu dhidi ya makafiri isipokuwa tu katika hali moja: ikiwa makafiri hawa wana ahadi kwa waislamu. Katika hali hii haijuzu kwetu kuwasaidia waislamu dhidi yao. Ni vipi kwa yule mwenye kuwasaidia makafiri juu ya kuwateketeza waislamu? Hili ni jambo lisilojuzu. Yote haya ni kwa ajili ya kutekeleza ahadi.

[1] al-Bukhaariy (3166).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 160
  • Imechapishwa: 19/02/2019