121. al-Qummiy upotoshaji wake wa nne wa al-An´aam


al-Qummiy amesema:

“Ja´far bin Muhammad ametuhadithia: ´Abdul-Kariym bin ´Abdir-Rahmaan ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin ´Aliy, kutoka kwa Muhammad bin al-Fadhwl, kutoka kwa Abu Hamzah aliyesema: “Nilimuuliza Abu Ja´far kuhusiana na maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُواiبِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ

“Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo, Tuliwafungulia milango ya [anasa za] kila kitu… “

Kuhusiana na maneno Yake:

فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ

“Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo… “

bi maana wakati walipoacha uongozi wa ´Aliy ambao wameamrishwa kushikamana nao. Ama kuhusiana na maneno Yake:

فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ

“… Tuliwafungulia milango ya [anasa za] kila kitu… “

bi maana nchi yao duniani na yale waliyofunguliwa. Kuhusu maneno Yake:

حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ

“… mpaka walipofurahia kwa yale waliyopewa; tamahaki Tukawachukua [kwa kawaadhibu], basi mara wao wakawa wenye kukata tamaa.”

bi maana kujitokeza kwa al-Qaa´im[1].  Mambo yatakuwa kama kwamba hawajapatapo kuwa na kiongozi kamwe. Hiyo ndio maana ya maneno Yake “tahamaki”. Aayah hii imeteremka kuhusiana na yeye:

فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Basi ikakatwa mizizi ya watu waliodhulumu. – Himdi zote anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.”[2]

Watu hawa ni watenda madhambi na wapumbavu wakubwa. Aayah hizi zimeteremka Makkah na zinazungumzia nyumati zilizotangulia ambazo ziliwakadhibisha Mitume watukufu. Allaah anazitaja khabari zao katika Aayah hizi kwa ajili ya mawaidha na ili wengine wapate mazingatio. Sambamba na hilo watenda madhambi hawa wapumbavu wanazipindisha kwenda katika ugomvi wa kisiasa juu ya mambo yanayohusiana na utawala kati ya kizazi cha Faatwimah na Maswahabah na Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Allaah kweli ameikata mizizi ya watu ambao wanakadhibisha adhabu kama vile mafuriko, ukelele na kutuma upepo ili wengine waweza kupata mazingatio. Mpumbavu huyu anasema kuwa adhabu hizi zitawapata Maswahabah, Banuu Umayyah na Banuul-´Abbaas wakati atapojitokeza al-Qaa´im. Hayo ni mambo ambayo kamwe hayatatokea. Si jengine isipokuwa ni katika ukhurafi wao na pumba zao.

[1] Mahdiy.

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/200).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 178-179
  • Imechapishwa: 12/06/2018