12. Msingi wa nne: Ubainifu wa elimu na wanazuoni

wanaShaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimhu Allaah) amesema:

Msingi wa nne:

Kubainisha elimu na wanazuoni, Fiqh na wanazuoni wa Fiqh [Fuqahaa´], na ubainifu wa yule mwenye kujifananisha na wao ilihali si katika wao.

MAELEZO

Kubainisha elimu na wanazuoni… – Huu ni msingi mkubwa ambao unazungumzia ni nini makusudio ya elimu. Makusudio ya ´elimu` ni elimu ya dini iliyojengwa juu ya Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio elimu yenye manufaa.

Ama kuhusu elimu ya kimazingira katika kazi za mikono, viwanda, udaktari na nyinginezo haisemwi kuwa ni `elimu` kwa njia ya kutofungamanisha. Kunaposemwa ´elimu` na ambayo iko na fadhila, basi makusudio ni elimu ya Kishari´ah. Ama elimu ya kazi za mikono, viwanda na fani mbalimbali, hizi ni elimu zenye kuruhusiwa na kuhalalishwa. Hata hivyo haisemwi kuwa ni ´elimu` pasi na kufungamanisha. Husemwa ´elimu ya uhandisi`, ´elimu ya udaktari` n.k. Lakini kwa masikitiko makubwa katika desturi za watu leo kunaposemwa ´elimu` basi wanafahamu kuwa ni elimu ya Hadiyth na wanasema unaposikia kitu katika Qur-aan basi kitu hicho kinafahamishwa na elimu ya Hadiyth kama ambavyo kunapokuja Hadiyth vilevile wanasema kuwa Hadiyth hiyo inajulishwa na elimu. Elimu za kazi za mikono, viwanda, udaktari na mengineyo hii leo ndio yanayoitwa kuwa ni ´elimu` licha ya kwamba mambo haya yanaweza kuwa ujinga kwa vile yanaweza kuingiliwa na makosa mengi kwa sababu ni ijitihada zinazofanywa na mtu. Hili ni tofauti na elimu ya Kishari´ah ambayo ni yenye kutoka kwa Allaah. Elimu hii:

لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ

“Haitokifikia ubatili mbele yake na wala nyuma yake; ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima, anayestahiki kuhimidiwa.” (41:42)

Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika si venginevyo wanaomkhofu Allaah [kikweli kweli] miongoni mwa waja Wake ni wanazuoni.” (35:28)

Makusudio hapa ni wasomi wa Shari´ah ambao wanamjua Allaah (´Azza wa Jall). Kuhusiana na wasomi wa uhandisi, mambo ya viwanda, uvumbuzi na udaktari, hawa wanaweza kuwa hawatambui haki ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) na hawamtambui Allaah. Utambuzi wao ni mfinyu. Wasomi wanaomtambua Allaah ni wale wanazuoni wa Shari´ah. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika si venginevyo wanaomkhofu Allaah [kikweli kweli] miongoni mwa waja Wake ni wanazuoni.”

Hili ni kwa sababu wanamtambua Allaah kwa majina na sifa Zake na vilevile wanajua haki Yake (Subhaanahu wa Ta´ala). Haya hayapatikani kwa kusoma elimu ya udaktari na uhandisi. Kinachoweza kupatikana kwa kusoma elimu hizo ni kujua Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah peke yake. Kuhusiana na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah inajulikana kwa kusoma elimu ya Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 28-30wa
  • Imechapishwa: 18/05/2021