12. Malaika wanailinda Shaam


84- Imaam Ahmad, at-Tirmidhiy na al-Haakim wamepokea kupitia kwa Zayd bin Thaabit aliyesema:

“Tulikuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tukiikusanya Qur-aan. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Twuubaa kwa Shaam!” Tukasema: “Kwa nini, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Hakika Malaika wa Mwingi wa huruma wananyoosha mbawa zao juu yake.”

at-Tirmidhiy amesema:

“Nzuri, Swahiyh na geni.”

al-Haakim amesema:

“Ni Swahiyh kwa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.”

85- Waathilah bin al-Asqa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Malaika wanaufunika mji wenu huu – bi maana Dameski – usiku wa ijumaa. Inapofika asubuhi wanatawanyika katika milango ya Dameski wakiwana bendera na mabango yao na … Halafu wanapanda juu na kuwaombea kwa Allaah: “Waponye wagonjwa wao! Warudhie yule waliyempoteza!”

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 10/02/2017