Ingawa baadhi ya wale walioishi karibu na zama za Ahmad walipatikana ambao walitumbukia katika kitu katika hayo kwa mujibu wa madhehebu ya Muqaatil, hawatoigilizwa katika jambo hilo. Wanaotakiwa kuigilizwa ni maimamu wa Uislamu kama vile Ibn-ul-Mubaarak, Maalik, ath-Thawriy, al-Awzaa´iy, ash-Shaafi´iy, Ahmad, Ishaaq na Abu ´Ubayd. Wote hawa hakupatikani katika maneno yao kitu katika sampuli ya maneno ya mutakallimiyn, seuze maneno ya wanafalsafa. Hakuna yeyote aliyesalimika na kupondwa na kujeruhiwa aliingia katika kitu katika hayo. Abu Zur´ah ar-Raaziy amesema:

“Msiwe na chochote kuhusiana na mtu ambaye yuko na elimu na asiilinde elimu yake na akahitajia kitu katika falsafa ili aweze kuieneza.”

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 56
  • Imechapishwa: 20/09/2021