12. Jina zuri linampa mtoto utukufu na fakhari


Jina zuru linampa mtoto utukufu na kujifakhari. Pindi mtoto anapofikisha miaka tano au sita kutaulizwa swali lifuatalo:

“Ni kwa nini umeniita hivyo? Kwa nini umenichagulia jina hilo? Maana yake nini?”

Hapo ndipo baba atafurahi ikiwa kama alimchagulia jina zuri. Au huanguka hali ya kufedheheka mbele ya mwanawe ikiwa alimchagulia jina baya. Hapa na pale ndipo kunafichuka upurukushani na upumbavu wa baba. Inakuwa katika ngazi ya malezi kitu cha kwanza baba alichofanya ni kumvisha mtoto wake vazi la kigeni na kumuweka katika hali isiokuwa nzuri. Huku ni kupinda na uongofu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipatia pindi aliposema:

“Hakuna mtoto yoyote isipokuwa huzaliwa katika maumbile. Baba yake ndio humfanya akawa myahudi, mkristo au mwabudu moto.”[1]

[1] al-Bukhaariy (3/176) na Muslim (2658).

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 13
  • Imechapishwa: 18/03/2017