117. Wachunga wakiwa miguu peku na wakishindana kujenga mijengo mirefu


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

na utaona wachunga wanaenda miguu chini, uchi na mafukara wakishindana kujenga majumba marefu.” 

MAELEZO

Miguu chini – Ni yule ambaye hana viatu.

Wachunga… – Ni wale wanaochunga kondoo na mbuzi. Watu hawa hapo kabla walikuwa kwenye majumba maporini wakihama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Zama za mwisho wataishi katika miji wakijenga majumba ya kifakhari na majengo marefu. Hii ni miongoni mwa alama za Qiyaamah. Watu wa mashambani watageuka kuwa watu wa kisasa, wakawa ni wenye kujenga majumba marefu na wakifakharishana na kusimbuliana, jambo ambalo sio katika ada yao, wakawa matajiri na watu wa maendeleo, hii ni katika alama za Qiyaamah.

Kama mnavojua Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hazungumzi kwa matamanio yake. Mnajua wenyewe hivi sasa ni vipi ziko hali za watu. Hali zimebadilika na mafukara wamegeuka kuwa matajiri, mashamba yamekuwa miji ya kisasa kwa sababu ya kujengwa na kurefusha majengo. Haya ni ukweli wa yale aliyosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 237-238
  • Imechapishwa: 02/02/2021