110. al-Qummiy upotoshaji wake wa pili wa al-Maa-idah


al-Qummiy amesema alipokuwa akifasiri Aayah:

الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ

“Leo wamekata tamaa wale waliokufuru juu ya dini yenu, hivyo basi msiwaogope na niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni Uislamu uwe dini yenu.”[1]

“Hapa ni pale ulipoteremshwa uongozi wa kiongozi wa waumini.”[2]

Iko wapi Aayah, au Aayaat, zinazotaja uongozi huu? Ziliteremshwa lini? Ni wapi zilipoteremshwa? Si ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) wala watu wa nyumbani hawazitambui. Vivyo hivyo Maswahabah na waumini wengine wote wa ulimwenguni katika historia ya Kiislamu. Lakini madai kama haya hayatoki kwengine isipokuwa ni kwa Ibn Sabaa´ myahudi. Tunawapongeza Raafidhwah Baatwiniyyah juu ya utukufu huu!

Isitoshe Aayah hii ni moja katika hoja kubwa dhidi ya Raafidhwah Baatwiniyyah ambao wanawatuhumu Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba wameritadi na kukufuru. Maana ya Aayah ni kwamba makafiri wamekata tamaa juu ya kuubatilisha Uislamu na kuwarudisha waislamu katika kufuru na shirki. Allaah (Ta´ala) amekokoteza hilo kwa kusema:

فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ

“… hivyo basi msiwaogope na niogopeni Mimi.”

Bi maana msikhofu kuwa watakushindeni au wataibatilisha dini yenu[3]. Hivyo ndivyo walivyokuwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) japokuwa watachukia Raafidhwah na Baatwiniyyah.

[1] 05:03

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/162).

[3] Tazama ”Fath-ul-Qadiyr” (2/15).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 157
  • Imechapishwa: 23/04/2018