11. Khatari ya kuwa na ´Aqiydah mbovu iliyopinda

Kuhusu Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wako katika njia iliyonyooka ni mamoja inapokuja katika maudhui haya na maudhui mengine yote ya dini. Hata hivyo inapokuja katika ´Aqiydah ni wenye kuitilia mkazo na umuhimu zaidi. Hilo si kwa jengine ni kwa sababu upotevu katika suala hili umekuwa ni mwingi na kukosea katika suala hili ni jambo la khatari na wengi wameteleza na kufahamu vibaya. Kukosea katika ´Aqiydah sio kama kukosea katika mambo mengine. Ambaye anakosea katika ´Aqiydah kunachelea juu yake akapatwa na ukafiri na upindaji mkubwa na upotevu wa hali ya juu. Ama yule mwenye kukosea katika jambo jingine ni sahali ingawa makosa yote katika dini hayajuzu.

Haijuzu kwa mtu akaendelea juu ya kosa au akamfuata kichwa mchunga mwenye kukosea. Lakini hata hivyo makosa yanatofautiana. Kosa la khatari zaidi ni katika ´Aqiydah. Upotevu katika ´Aqiydah ndio mbaya zaidi. Kukosea katika mambo mengine yasiyokuwa ´Aqiydah yanaingia ndani ya utashi tofauti na ´Aqiydah:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah, basi kwa hakika amepotoka upotofu wa mbali.”[1]

Katika Aayah nyingine amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah, basi kwa hakika amezua dhambi kuu.”[2]

[1] 04:116

[2] 04:48

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mujmal ´Aqiydat-is-Salaf as-Swaalih, uk. 11
  • Imechapishwa: 24/05/2022