11. Jina linafahamisha mengi


Ee Muislamu! Allaah akubarikie mtoto wako aliyekuruzuku! Jitahidi uwe ni mzuri kwa mwanao, kwako mwenyewe na Ummah wako kwa kuchagua jina zuri kimatamshi na kimaana. Uchaguzi mzuri unafahamisha mengi zaidi ya kitu kimoja tu. Unafahamisha namna ambavyo baba amevyoshikamana na uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Unafahamisha namna fikira zake zilivyo. Jina linaabiria maumbile ya yule mtoaji jina na kufichua uelewa wake. Katika maneno ya watu husemwa:

“Nimemjua baba yako kupitia jina lako.”

Jina linamfungamanisha mtoto na uongofu na adabu za Kishari´ah. Hivyo mtoto anakuwa ni mwenye kubarikiwa na siku zote jina lake hukumbushia jina la Mtume au mja mwema. Matokeo yake anapata fadhila za du´aa na kuanza kuwaiga wema waliotangulia (Salaf-us-Swaalih). Majina yao yanahifadhiwa na siku zote anakumbushia sifa na hali zao. Namna hii ndiyo unaendelea mlolongo katika vizazi.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 12-13
  • Imechapishwa: 18/03/2017