11. Dalili ya tisa kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


9- Shaykh Swaalih Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Ahmad bin an-Naquur al-Bazzaaz ametukhabarisha: Abu Twaalib ´Abdul-Qaadir bin Muhammad al-Yuusufiy ametuhadithia: Abu ´Aliy al-Mudhahhib ametuhadithia: Abu Bakr al-Qatwi´iy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Ahmad ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia: Muhammad bin Fudhwayl ametuhadithia: ´Umaarah bin al-Qa´qaa´ ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Abiy Nu´aym, kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy aliyesema:

“Baada ya ´Aliy kupigana alimtumia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) dhahabu kutoka Yemen ambayo bado haijasafishwa kutoka kwenye udongo wake aliokuwa kwenye mfuko wa ngozi ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaigawanya kati ya watu wane: Zayd al-Khayr, al-Aqra´ bin Haabis, ´Uyaynah bin Hiswn, ´Alqamah bin ´Ilaaqah – au Amr bin at-Twufayl (´Umarah alitilia shaka). Ikapelekea baadhi ya Maswahabah wake, ´Answaar na wengineo, wakachukulia vibaya, ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Hivi kweli hamniamini ilihali naaminiwa na Yule aliye mbingun? Najiwa na khabari kutoka kwa Yule aliye mbinguni asubuhi na jioni.” Ndipo akasogea mbele yake mwanaume ambaye alikuwa na macho yaliyoingia kwa ndani, mwenye taya zilizochomoza na paji la uso lililoinuka. Akasema: “Ee Mtume wa Allaah, mche Allaah!” Akasema  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akainua kichwa chake, akamtazama na kusema: “Ola wako! Je, mimi si ndiye katika walioko ardhini ambaye nina haki zaidi ya kumcha Allaah?”Mtu yule akaenda zake. Khaalid akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Si nimkate shingo yake?” Akasema: “Huenda anaswali.”Khaalid akasema: “Huend kweli anaswali, anasema kwa ulimi wake asiyoyaamini moyoni mwake.”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mimi sikuamrishwa kuzichimba nyoyo za watu wala kuyapasua matumbo yao.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamtazama na kusema: “Kutokea kwa huyu watatokea watu ambao wanaisoma Qur-aan pasi na kuvuka koromeo zao. Wanatoka katika dini kama ambavyo mshale unavotoka kwenye upinde wake.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim katika “as-Swahiyh” zao.

al-Bukhaariy ameipokea kupitia kwa Qutaybah bin Sa´iyd kutoka kwa ´Abdul-Waahid bin Ziyaad kutoka k wa ´Umaarah bin al-Qa´qaa´.

Muslim ameipokea kupitia kwa  Ibn Numayr kutoka kwa Muhammad bin Fudhwayl kutoka kwa ´Umaarah kutoka kwa Ibn Abiy Nu´m ambaye jina lake ni ´Abdur-Rahmaan.

[1] al-Bukhaariy (3610, 3344, 4351 na 7433), Muslim (1064) na Abu Daawuud (4764).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 80-82
  • Imechapishwa: 16/04/2018