107. al-Qummiy upotoshaji wake wa kumi na sita wa an-Nisaa´


al-Qummiy amesema alipokuwa akifasiri Aayah:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا

“Enyi watu!  Hakika imekujieni burhani kutoka kwa Mola wenu na tumekuteremshieni Nuru ya wazi kabisa.”[1]

Nuru kunamaanishwa kiongozi wa waumini. Kisha akasema:

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَاعْتَصَمُوا بِهِ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِي رَحْمَةٍ مِّنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا

“Ama wale waliomuamini Allaah na wakashikamana Nayem, basi atawaingiza katika rehema kutoka Kwake na fadhila na atawaongoza Kwake njia iliyonyooka.”[2]

Ni wale walioshikamana barabara na uongozi wa kiongozi wa waumini na wa maimamu.”[3]

Kusema kwamba nuru ni kiongozi wa waumini ni kumsemea na kumzulia Allaah uongo mbaya kabisa na Kitabu Chake. Makusudio ya nuru ni Qur-aan hii ambayo Allaah amemwongoza kwayo Mtume Wake na waumini na khaswa khaswa Maswahabah watukufu akiwemo ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum).

Wale walioamini na wakashikamana barabara na Allaah na Kitabu Chake ni Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale waliowafuata kwa wema, na sio Raafidhwah na Baatwiniyyah ambao wamezua uongozi huu. Ukweli wa mambo ni kwamba ´Abdullaah bin Sabaa´ myahudi ndiye aliyewazulia. Yeye ndiye aliyewazulia Raafidhwah na Baatwiniyyah dini kama ambavo Paulo aliwazulia dini manaswara.

[1] 04:174

[2] 04:175

[3] Tafsiyr al-Qummiy (1/159).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 153
  • Imechapishwa: 13/04/2018