Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا

“Atakayemtii Allaah na Mtume hao watakuwa pamoja na wale Allaah aliowaneemesha – Manabii na wakweli na mashahidi na waja wema – na uzuri ulioje hao kuwa ni rafiki!” 04:69

Qataadah amesema:

“Kuna baadhi ya Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walimuuliza: “Ni vipi hali itakuwa Peponi ilihali wewe utakuwa katika daraja ya juu na sisi tutakuwa chini yako? Vipi tutakuona?” Ndipo Allaah (Ta´ala) akateremsha Aayah hii:

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ

“Atakayemtii Allaah… “

Bi maana katika kutekeleza faradh

وَالرَّسُولَ

“… na Mtume… “

Bi maanaa katika mambo yaliyopendekezwa.

فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ

“… hao watakuwa pamoja na wale Allaah aliowaneemesha – Manabii… “

Bi maana hawatopitwa na kuwaona Mitume na kutangamana nao. Daraja iliyo juu kabisa kwa wanaadamu ni ya Mitume. Kisha kunafuatia ya wakweli, mashahidi na waja wema. Mpangilio huu hauna shaka yoyote. Allaah (Ta´ala) amewataja kwa mpangilio na akaanza na Mitume kisha wale wenye kuwafuatia na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 225
  • Imechapishwa: 17/12/2016