104. al-Qummiy upotoshaji wake wa kumi na tatu wa an-Nisaa´


al-Qummiy amesema wakati alipokuwa akiifasiri Aayah:

وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ جَامِعُ الْمُنَافِقِينَ وَالْكَافِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا

“Hakika mmeshateremshiwa katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa mzaha, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Vinginevyo mtakuwa kama wao. Hakika Allaah atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Moto.”[1]

Aayah za Allaah ni Qur-aan ambayo Allaah ameiteremsha kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kuwaongoza watu. Ambazo ziko na Tawhiyd na kuipiga vita shirki, upotevu, ujinga, kubainisha yaliyo ya halali na yaliyo ya haramu na tabia njema na kutahadharisha uongo na kumzulia Allaah uongo na kukipotosha Kitabu Chake, kama wafanyavyo mayahudi. Kadhalika Raafidhwah wanafuata nyayo za mayahudi.

Wale wanaozifanyia mzaha Aayah za Allaah walikuwa ni makafiri wa Makkah na al-Madiynah  kabla hata maimamu hawajazaliwa. Wale wanaozichezea shere Aayah za Allaah baada ya kufa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Raafidhwah Baatwiniyyah. Ni mara ngapi wanazichezea shere Aayah za Allaah kukiwemo mzaha huu ambao tumeufichua hapa! Si washirikina, mayahudi wala maadui wengine wa Allaah hakuna ambao wamezifanyia mzaha Aayah za Allaah sana kama walivofanya hawa Raafidhwah Baatwiniyyah!

[1] 04:140

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 151-152
  • Imechapishwa: 12/01/2018