103. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kumi na moja wa an-Nisaa´

al-´Ayyaashiy amesema wakati alipokuwa akifasiri Aayah:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا ثُمَّ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ سَبِيلًا

“Hakika wale walioamini kisha wakakufuru halafu wakaamini kisha wakakufuru, kisha wakazidi kufuru, Allaah hatowasamehe na wala hatowaongoa njia.”[1]

“´Abdur-Rahmaan bin Kathiyr al-Haashimiy amesimulia kwamba Abu ´Abdillaah amesema: “Imeteremshwa juu ya fulani na fulani. Mara ya kwanza walimuamini Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha wakakufuru wakati walipoonyeshwa uongozi. Aliposema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule ambaye mimi ni kipenzi wake basi ´Aliy vilevile ni kipenzi wake.”

Halafu wakaamini kiapo cha utiifu kwa kiongozi wa waumini na wakampa kiapo cha usikivu na utiifu. Pindi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofariki wakakufuru na wakakanusha kiapo cha usikivu na utiifu. Uhakika wa mambo wakazidi kufuru pale walipopokonya uongozi kutoka kwake. Hawakubali na imani yoyote kabisa.”[2]

Namna hii ndivyo wafanyavyo Baatwiniyyah maadui wa Allaah; wanamkufurisha Abu Bakr as-Swiddiyq, ´Umar al-Faaruq na Maswahabah wengine wote (Radhiya Allaahu ´anhum) wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao Allaah aliunyanyua Uislamu kupitia wao na akawatokomeza washirikina, waabudu moto, mayahudi, manaswara na wenye kuritadi.

[1] 04:137

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/281).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 151
  • Imechapishwa: 10/01/2018