100. Sura ya nne: Kuzungumzia mifano ya Bid´ah za kisasa

Bid´ah za kisasa ni nyingi kwa sababu ya zama kwenda zaidi, uchache wa elimu, walinganizi wengi wanaolingania katika Bid´ah na mambo yenye kwenda kinyume, uharaka wa kujifananisha na makafiri katika desturi na mila zao. Hayo yanathibitisha yale ambayo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Hakika mtafuata njia za wale waliokuwa kabla yenu.”[1]

Miongoni mwa Bid´ah hizo ni hizi zifuatazo:

1- Kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

2- Kufanya Tabarruk kwa maeneo, athari, wafu na mfano wake.

3- Bid´ah katika uwanja wa ´ibaadah na kujikurubisha kwa Allaah.

[1] Ahmad (21947) na tamko ni lake na at-Tirmidhiy (2185).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 191-192
  • Imechapishwa: 09/07/2020