10. Wanawasifia Ahl-ul-Bid´ah na kuwakaripia Ahl-us-Sunnah

10- Kuyaweka mambo pasipokuwa mahali pake pa Kishari´ah na pa sawa. Mfano wa hilo wanawasifia Ahl-ul-Bid´ah na kuwanyanyua angani na harakati zao ilihali wanawakaripia wale wenye kustahiki kusifiwa, kutapwa na kuombewa du´aa kwa sababu wanafanya vichinjo vikubwa na kuendelea kupita juu ya njia ya kheri na uongofu wa kiutume uliyonyooka.[1]

[1] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)

 

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 20
  • Imechapishwa: 25/03/2017