10. Tone kidogo la damu katika masiku ya ada


Swali 10: Wakati fulani mwanamke anaona athari ndogo ya damu au tone kidogo sana linaloenea katika masaa ya mchana. Mara anaiona wakati wa ada yake lakini haishuki na mara nyingine anaiona kipindi ambacho sio cha ada yake. Ni ipi hukumu ya funga yake kaitka hali zote mbili?

Jibu: Punde kidogo tumetangulia kujibu swali mfano wa hili. Lakini kuna nukta iliyobaki; akiona tone hili ni katika masiku ya ada yake na yeye anaizingatia kuwa ni hedhi kutokana na anavoitambua, basi tone hilo litakuwa ni hedhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 13
  • Imechapishwa: 19/06/2021