Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

05- Hapana mungu wa haki asiyekuwa Yeye.

MAELEZO

Hii ndio Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Kusema kwamba hapana mungu wa haki asiyekuwa Yeye maana yake ni kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Hata hivyo ni kosa kusema kwamba hakuna anayeabudiwa mwengine asiyekuwa Allaah. Wako wengi wanaoabudiwa badala ya Allaah (´Azza wa Jall). Unaposema kuwa hakuna mwengine anayeabudiwa badala ya Allaah, ina maana kwamba vile vyengine vyote vinavyoabudiwa ni Allaah. Hivi ndivo wanavyoamini watu wa Wahdat-ul-Wujuud. Mwenye kusema na kuamini hivo ni katika Wahdat-ul-Wujuud. Lakini ikiwa anasema pasi na kuamini hivo, bali ni kwa sababu ya ujinga au kufuata kibubusa, ametamka makosa na ni wajibu kurekebisha. Baadhi ya watu huzianza swalah kwa kusema:

“Hakuna mwengine mwenye kuabudiwa asiyekuwa Yeye.”

Allaah pekee ndiye mwenye kuabudiwa kwa haki. Wengine wote wanaoabudiwa ni batili. Amesema (Ta´ala):

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ

“Hivyo ni kwa kuwa Allaah ndiye wa haki na kwamba vile wanavyoomba badala Yake ndiyo batili na kwamba Allaah ndiye Aliye juu kabisa, Mkubwa.”[1]

[1] 22:62

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 13/06/2019