10. Mke mwema anatakiwa kumheshimu mume wake

Katika sifa za mke mwema ni kwamba anamuheshimu mume wake na anajua nafasi yake na haki zake. Kumekuja Hadiyth nyingi kuhusu hili. Moja wapo ni yale aliyopokea at-Twabaraaniy katika “al-Muj´am al-Kabiyr”[1] kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Simwamrishi yeyoye kumsujudia mwingine. Lau ningelimwamrisha yeyote kumsujudia mwingine, basi ningelimwamrisha mwanamke kumsujudia mume wake.”

at-Twabaraaniy amepokea katika “al-Muj´am al-Kabiyr”[2] kupitia Zayd bin Arqam kwamba Mu´aadh amesema:

“Ewe Mtume wa Allaah! Watu wa kitabu wanawasujudia maaskofu na wakuu wao; je, tusikusujudie?” Akasema: “Lau ningelimwamrisha yeyote amsujudie mwingine, basi ningelimwamrisha mwanamke kumsujudia mume wake. Mwanamke hakutimiza haki za mume wake mpaka pale ambapo atakapomuomba kufanya naye jimaa wakati yeye atakuwa ameketi juu ya tandiko dogo na akamtii.”

Haki za mume zinakuwa maradufu ikiwa ni mwema, mchaMungu, mtu wa dini na anahifadhi ´ibaadah za Allaah na kumtii. at-Tirmidhiy na Ibn Maajah wamepokea kupitia kwa Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mwanamke ambaye anamuudhi mume wake duniani isipokuwa mke wake katika al-Huur al-´Ayn anasema: “Usimuudhi, Allaah Akuue! Huyo kwako ni mgeni tu. Karibuni atakuacha na kuja kwetu.”[3]

Wanachuoni wanasema kwamba katika Hadiyth hii kuna matishio makali kwa wanawake wanaowaudhi waume zao.

[1] 11/356. Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika ”as-Swahiyhah” (3490).

[2] 5/207. Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika “as-Swahiyhah” (3366)

[3] at-Tirmidhiy (1174) na Ibn Maajah (2014). Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika ”as-Swahiyhah” (173).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 40
  • Imechapishwa: 05/08/2018