10. Kuoga ndio bora zaidi kuliko kutawadha


8- Kuoga ndio bora zaidi

Lakini hata hivyo kuoga ndio bora zaidi kuliko kutawadha kutokana na Hadiyth ya Abu Raafi´ aliyesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuna siku moja aliwazungukia wakeze na akawa anaoga kwa huyu na kwa huyu. Nikamwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Kwa nini usifanye kuoga mara moja tu?” Akasema: “Kufanya hivi ndiko kutakasifu zaidi, nzuri zaidi na safi zaidi.”[1]

[1] Ameipokea Abu Daawuud, an-Nasaa´iy katika “´Ishrat-un-Nisaa´” (01/79), at-Twabaraaniy (01/96/06), Abu Nu´aym katika “at-Twib” (01/12/02) kwa mlolongo wa wapokezi mzuri. Ameipa nguvu al-Haafidhw. Tayari nimeishaizungumzia katika “Swahiyh Sunan” kwa nambari. 215.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 107-108
  • Imechapishwa: 08/03/2018