Neno hili likisemwa kwa ukweli, kwa kumtakasia nia Allaah na mtu akatendea kazi yale inayopelekea kwa nje na kwa ndani lina athari zenye kusifiwa kwa mtu binafsi na kwa jamii. Miongoni mwa athari hizo ni zifuatazo:

1 – Waislamu wanakuwa na umoja ambao unapelekea kupata nguvu na kuwashinda maadui wao. Kwa sababu watakuwa wanaamini dini moja na ´Aqiyda moja. Amesema (Ta´ala):

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

“Shikamaneni nyote kwa pamoja kwa kamba ya Allaah na wala msifarikiane.” (03:103)

هُوَ الَّذِي أَيَّدَكَ بِنَصْرِهِ وَبِالْمُؤْمِنِينَ وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ ۚ لَوْ أَنفَقْتَ مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مَّا أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

”Yeye ndiye ambaye Kakusaidia kwa nusura Yake na kwa waumini na akaziunganisha nyoyo zao. Lau ungelitoa vyote vilivyomo ardhini, basi usingeliweza kuunganisha nyoyo zao, lakini Allaah ndiye kawaunganisha. Hakika Yeye ni Mwenye nguvu asiyeshindika, Mwenye hekima.” (08:62-63)

Kufarikiana, mizozo na mivutano ndio sababu imepelekea katika ´Aqiydah. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ

“Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundi makundi, huna lolote kuhusiana nao.” (06:159)

فَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ زُبُرًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

“Lakini wakalivunja jambo lao kati yao makundi mbalimbali, kila kundi linafurahia yale waliyokuwa nayo.” (23:53)

Hakuna kingine kinachowafanya watu kuwa na umoja isipokuwa ´Aqiydah, imani na kumwabudu Allaah pekee ambayo ndio yenye kufahamishwa na shahaadah. Waarabu walielewa hivo kabla ya Uislamu na baada yake.

2 – Jamii inayotendea kazi kwa mujibu wa shahaadah unakuwa na amani na utulivu. Kwa sababu kila mmoja atakuwa ni mwenye kutendea kazi yale Allaah aliyomhalalishia na kuacha yale Allaah aliyomharamishia kwa mujibu wa ´Aqiydah yake. Matokeo yake anajizuia kutokamana na unyanyasaji, dhuluma na uadui na badala yake ushirikiano, mapenzi na kupenda kwa ajili ya Allaah ndio vinachukua nafasi ya hayo kwa kutendea kazi maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ

“Hakika si vyengine waumini ni ndugu.” (49:10)

Haya yanapata kudhihirika wazi kwa kuiangalia hali ya waarabu kabla na baada ya kuamini neno hili. Hapo kabla walikuwa ni maadui wenye kujifakhirisha kwa kuua, kupora na kuiba. Walipojisalimisha nalo wakawa ni ndugu wenye kupendana. Amesema (Ta´ala):

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ

“Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni washupavu zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao.” (48:29)

وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا

“Kumbukeni neema ya Allaah juu yenu pale mlipokuwa maadui kisha akaunganisha nyoyo zenu na mkawa kwa neema Yake ndugu.” (03:103)

3 – Kupata mamlaka, uongozi katika ardhi, dini inasafika na kuwa na uimara mbele ya mikondo, fikira na misingi mbalimbali. Amesema (Ta´ala):

وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًاۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا

“Allaah amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema ya kwamba atawafanya kuwa makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wale waliokuwa kabla yao, na atawamakinishia dini yao aliyowaridhia na atawabadilishia amani badala ya khofu yao; [kwa sharti] wananiabudu Mimi pekee na wasinishirikishe na chochote.” (24:55)

Amefungamanisha (Subhaanah) kufikia malengo haya makubwa kwa kumuabudu Yeye pekee asiyekuwa na mshirika, jambo ambalo ndio maana na inavyopelekea shahaadah.

4 – Mwenye kusema ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” na akatendea kazi yale inayopelekea basi anapata raha na utulivu wa moyo na akili. Kwa kuwa anakuwa ni mwenye kumwabudu Mola Mmoja ambaye anajua malengo Yake na yale yenye kumridhisha akayafanya na anajua yale yenye kumuudhi na hivyo akawa mwenye kuyaepuka. Hili ni tofauti na yule ambaye anawaabudu waungu wengi. Kila mmoja katika wao ana malengo yake na anataka kuendesha mambo kinyume na anavyotaka mwengine. Amesema (Ta´ala):

أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ

“Je, waungu wengi wanaofarakana ni bora au Allaah; Mmoja pekee, Aliyeshinda juu kabisa?” (12:39)

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلًا فِيهِ شُرَكَاءُ مُتَشَاكِسُونَ وَرَجُلًا سَلَمًا لِّرَجُلٍ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا

“Allaah amepiga mfano wa mtu aliyekuwa na washirika wagombanao na mtu mwengine aliyesalimika na bwana mmoja tu. Je, wanalingana sawa kwa hali zao?” (39:29)

Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Huu ndio mfano Allaah (Subhaanah) amempigia mshirikina na yule mwenye kumuabudu Allaah peke yake. Mshirikina ni kama mtumwa anayemilikiwa na kundi la watu wanaovutana, wanaotofautiana na kugombana; yule mtumwa hawi kawaida. Mshirikina alipokuwa ni mwenye kuwaabudu waungu wengi anakuwa ni kama mtumwa anayemilikiwa na kundi la watu wenye kugombana ili awatumikie. Hawezi kuwaridhisha wote kwa wakati mmoja. Mpwekeshaji alipokuwa ni mwenye kumuabudu Allaah Mmoja anakuwa ni kama mtumwa wa bwana mmoja aliyejisalimisha kwake, akajua malengo yao na namna ya kumridhisha. Anakuwa katika raha kutokamana na kumgombania. Bali anakuwa amejisalimisha kwa bwana wake pasi na kugombaniwa. Isitoshe bwana huyo anakuwa ni mpole kwake, mwenye huruma, kumfanyia wema na kuyajali manufaa yake. Je, watumwa wawili hawa wako sawa?”[1]

5 – Watu wa shahaadah wanapata ukuu na utukufu katika dunia na Aakhirah. Amesema (Ta´ala):

حُنَفَاءَ لِلَّـهِ غَيْرَ مُشْرِكِينَ بِهِ ۚوَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ

“Mumwabudu Allaah Mmoja pasi na kumshirikisha; na yeyote anayemshirikisha Allaah ni kana kwamba ameporomoka kutoka mbinguni wakamnyakua ndege au upepo ukamtupa mahali pa mbali kabisa.” (22:31)

Aayah inafahamisha kuwa kwa Tawhiyd mtu anapata kuwa juu na kutukuka na kwa shirki mtu anapata kuwa chini na kutwezeka.

´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Allaah amefananisha ile heshima na utukufu [wa imani na Tawhiyd] ni kama vile mbingu ambayo ndio mahali pake pa kupandia na pa kushukia. Kutoka kwayo [imani na Tawhiyd hiyo] anashuka mtu katika ardhi na kwayo mtu anapanda. Amemfananisha vilevile yule mwenye kuacha imani na Tawhiyd ni kama mfano wa kuanguka chini kabisa kutoka mbinguni.”[2]

6 – Kusalimika kwa damu, mali na heshima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimeamrishwa kuwapiga vita watu mpaka watakaposema “Hapana mungu isipokuwa Allaah. Wataposema hivo imesalimima kwangu damu na mali yao isipokuwa kwa haki yake.””

Maneno yake:

“… kwa haki yake.”

ina maana kwamba watapoisema na wakaacha kuitendea haki yake ambayo ni ile Tawhiyd inayopelekea na kujitenga mbali na shirki na kutekeleza nguzo za Uislamu, basi haitosalimisha mali zao wala damu zao. Kinyume chake watatakiwa kupigwa vita na mali yao itafanywa kuwa ni mateka ya waislamu. Hivyo ndivyo alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na makhaliyfah wake.

Neno hili lina athari tutkufu kwa mtu binafsi na jamii katika mambo ya ´ibaadah, biashara, adabu na tabia.

Allaah ndiye Mwenye  kuongoza. Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah wake wote.

[1] I´laam-ul-Muwaqqi´iyn (01/187)

[2] I´laamul-ul-Muwaqqi´iyn (01/180).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´naa laa ilaaha illa Allaah, uk. 40-47
  • Imechapishwa: 23/09/2023