1 – Imaam na ´Allaamah ´Ubaydullaah ar-Rahmaaniy al-Mubaarakfuuriy (Rahimahu Allaah)

Amesema (Rahimahu Allaah) katika cheti chake cha Hadiyth kwa Shaykh Rabiy´ ambacho alimpa rukhusa ya kufundisha Hadiyth:

“Amma ba´d:

Mja wa Allaah fakiri Abul-Hasan ´Ubaydullaah ar-Rahmaaniy al-Mubaarakfuuriy[1], mtoto wa ´Allaamah na Shaykh ´Abdus-Salaam al-Mubaarakfuuriy ambaye ni mwandishi wa wasifu wa al-Bukhaariy, anasema:

Hakika ndugu yetu kwa ajili ya Allaah, mwanachuoni mtukufu na muheshimiwa, Shaykh Rabiy´ bin Haadiy ´Umayr al-Madkhaliy kutoka katika kijiji cha al-Jaraadiyyah wilaya ya Swaamitwah ya Saudi Arabia, mwalimu wa kitivo cha Hadiyth Chuo Kikuu cha Kiislamu al-Madiynah al-Munawwarah, ameniomba kumpa cheti cha rukhusa ya kufundisha Hadiyth. Ameniunganishia mnyororo wake wa wapokezi (Sanad) kwa mnyororo wa maimamu wa Hadiyth na miongoni mwa hao kuko walioandika vitabu Swahiyh na wengineo. Ameniandikia kwamba alisoma kwanza katika al-Madrasah as-Salafiyyah Swaamitwah. Kisha katika Chuo Kikuu cha elimu katika mji huohuo. Kisha katika Chuo Kikuu cha Kiislamu al-Madiynah al-Munawwarah na akapata shahada yake ya mwaka 1385. Mwaka wa 1396 akapata shahada yake ya pili. Mwaka wa 1400 akapata shahada yake ya udaktari kwenye Chuo Kikuu cha Mfalme ´Abdul-´Aziyz Juddah. Amenambia pia kuwa amesikiliza sana duruus za ´Allaamah na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Hafidhwahu Allaah) sehemu kubwa ya “Swahiyh al-Bukhaariy” na “Swahiyh Muslim” na sehemu ya “Sunan at-Tirmidhiy” kwenye msikiti mtukufu wa Mtume. Kadhalika amelazimiana sana na ´Allaamah na Shaykh Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Vilevile alifaidika kutoka kwa Shaykh Hammaad bin Muhammad al-Answaariy na wanachuoni wengine wakubwa. Baada ya kutoka katika Chuo Kikuu al-Madiynah, Chuo Kikuu kilimtuma kwenye Chuo Kikuu Salafiyyah cha Varanasi India kufundisha. Kila wakati nilipokuwa ninaenda katika Chuo Kikuu Salafiyyah baada ya kubaki kwake huko, alikuwa akikaa na mimi na kunikumbusha masuala ya kielimu. Alikuwa akija pia mara nyingi katika mji wa Mubaarakfuur na kunitembelea kwenye nyumba yangu. Nilikuta kuwa ana elimu kubwa. Ana fadhilah kubwa na ni mtu mwenye ufahamu uliosalimika na tabia iliyonyooka. Alikuwa amenyooka juu ya mfumo wa wema waliotangulia (Radhiya Allaahu ´anhum) katika I´tiqaad na matendo. Anafuata Kitabu na Sunnah, anavinusuru na kuvitetea. Alikuwa ni mwenye msimamo mkali kwa watu wa Bid´ah na watu wanaofuata matamanio yao (Ahl-ul-Bid´ah wal-Hawaa). Anawaraddi wanaofuata kipofu (Muqalliduun) ambao wanalinganisha Hadiyth na madhehebu ya maimamu wao. Allaah Ambariki katika elimu yake na Awafanye Waislamu wazidi kustarehe kwa urefu kwa kubakia kwake… “

Haya yameandikwa na Shaykh tarehe kumi na tisa Dhul-Qa´dah 1401.

[1] Ni mwandishi wa kitabu ”Mur´aat-ul-Mafaatih Sharh Mishkaat-il-Maswaabih”. Ni mmoja katika wanachuoni wenye kusifiwa India na bingwa wa wajuzi wa Hadiyth. Alifariki 1414. Kama jinsi alivyompa Shaykh Rabiy´ idhini na rukhusa ya kufundisha (Ijaazah), kadhalika alifanya hivo kwa Shaykh Hamuud at-Tuwayjiriy, Shaykh Ismaa´iyl al-Answaariy, Shaykh Ahmad an-Najmiy, Shaykh Badiy´-ud-Diyn as-Sindiy, Shaykh ´Aliym-ud-Diyn an-Nadyaawiy, Shaykh Muhammad as-Suumaaliy na wengineo. Allaah Awarahamu waliokufa katika wao na Awahifadhi waliohai.

  • Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
  • Imechapishwa: 28/11/2019