09. Ulipuaji wa Raafidhwah Makkah ni mfano wa ugaidi

8- Kwa hivyo matendo maovu ya genge dhalimu na yaliyopotoka wakati waliposhambulia msikiti Mtakatifu na wakaweka ndani yake vilipuzi vinavyoangamiza katika mnasaba wa hajj ya mwaka 1409 ni mfano wa ugaidi uliyopangwa kutoka sehemu ya mbali. Baada ya hapo njama na maandalizi hayo, kutoka kwa watu maluuni yakahamishwa kwenye msikiti Mtakatifu wa Allaah. Allaah amesema kuhusu nyumba hii:

وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُّذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ

“Yeyote anayekusudia humo kufanya upotevu kwa dhulma, basi Tutamuonjesha adhabu iumizayo.”[1]

Ndugu msomaji! Ukitaka kupata picha ya mbiombio na ya wazi ya magaidi hawa basi soma misitari ifuatayo:

“Ni genge ovu, lililopotoka, haribifu na la kipumbavu linalojinasibisha na kundi linalomfuata Khomeini. Wengi wao ni Raafidhwah. Walifanikiwa kuingiza mabomu Makkah wakati wa hija ya mwaka jana. Magaidi wenye chuki walipata mazoezi namna ya kuyatunza mabomu.”

Jioni tarehe 07 Dhul-Hijjah mwaka huo huo kulitokea mlipuko. Matokeo yake kukatokea khasara kubwa, akauwa mwanamume mmoja wa pakistani na watu kumi na sita wakajeruhika. Baadaye muda kidogo mhalifu akakamatwa na serikali ya kisaudia.

Wakaulizwa malengo yao juu ya matendo haya ya kigaidi. Magaidi hawa wakakubali wenyewe ya kwamba malengo yao ilikuwa kuwatisha mahujaji na kutikisa usalama wa kwenye mji mtakatifu. Aidha walikuwa wameahidiwa kupewa malipo kutoka kwa kiongozi wa ugaidi wa kisasa: Raafidhwah. Wakapewa malipo yao kwa mujibu wa matendo yao ya jinai. Wakahukumiwa na mahakama ya juu ya Kishari´ah ya Makkah; hawakuhukumiwa kwa sheria zilizotungwa na wanaadamu. Kumi katika wao ambao walikuwa wameshapata akili na wameshakomaa wakahukumiwa kuuawa tarehe 21 Swafar mwaka 1410. Waliosalia wakahukumiwa kufungwa jela na kuchapwa kwa sababu ya kushiriki kwao katika ulipuaji:

وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ

”Lakini vitimbi viovu havimzunguki isipokuwa mwenyewe.”[2]

وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا

“Na wala nafsi yoyote haitachuma isipokuwa ni juu yake.”[3]

[1] 22:25

[2] 35:43

[3] 06:164

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 03/04/2017