09. Sehemu kubwa ya Qur-aan ni Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat

Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat maana yake ni kumthibitishia Allaah (´Azza wa Jall) majina na sifa alizojithibitishia Mwenyewe na alizomthibitishia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sambamba na hilo umkanushie kasoro na mapungu ambayo Allaah amejikanushia Mwenyewe na alizomkanushia Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtu anatakiwa kufanya hivo pasi na kupotosha, kukanusha, kufanya namna na kufananisha. Amesema (Ta´ala):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Basi msimpigie mifano Allaah, kwani hakika Allaah anajua nanyi hamjui.”[2]

Vilevile inahusiana na yale yaliyotajwa katika Aayat-ul-Kursiy, Suurah “al-Ikhlaasw” na Suurah nyingi zilizoteremka Makkah ambazo zimetaja majina na sifa za Allaah. Vivyo hivyo Suurah zilizoteremka al-Madiynah. Sivyo tu, bali sehemu kubwa ya Qur-aan.

[1] 42:11

[2] 16:74

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mujmal ´Aqiydat-is-Salaf as-Swaalih, uk. 09-10
  • Imechapishwa: 24/05/2022