6- Anatakiwa azikwe ndani ya mji aliyofia na wala asisafirishwe kwenda mji mwingine. Kwa sababu kitendo hicho kinapingana na uharaka ulioamrishwa katika Hadiyth ya Abu Hurayrah iliotangulia. Mfano wake ni Hadiyth ya Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesema:

“Ilipotokea ile siku ya Uhud walibweba wauliwaji ili wakazikwe al-Baqiy´. Akanadi mwenye kunadi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakuamrisheni muwazike wauliwaji sehemu zao walipofia – baada ya kuwa mama yangu ameshambeba baba yangu na mjomba yangu wakiwa katika mbavu mbili za mnyama.”

Katika upokezi mwingine:

“… katika mbavu mbili za mnyama.” [juu ya ngamia] ili aende kuzikwa katika makaburi ya al-Baqiy´ – ambapo wakarudishwa.”

Katika upokezi mwingine:

“Tukawarudisha pamoja na wauliwaji palepale walipouliwa.”

Wameipokea wapokezi wa as-Sunan wanne, Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake (196-mawaarid) na huo upokezi mwingine ni wake, Ahmad (03/297-380), al-Bayhaqiy (04/57) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

Ziada ni ya Ahmad katika upokezi ambao tamko lake linakuja katika masuala ya kipengele cha 80.

Kwa ajili hiyo ´Aaishah amesema wakati alipokufa ndugu yake katika jangwa la Uhabeshi ambapo akachukuliwa kutoka mahali pake hapo:

“Hakuna ninachokichukia nafsini mwangu au kinachonihuzunisha nafsini mwangu isipokuwa mimi nilipendelea bora angezikwa mahali pake.”

Ameipokea al-Bayhaqiy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

an-Nawawiy amesema katika “al-Adhkaar”:

“Akiacha anausia asafirishwe kwenda mji mwingine, basi wasia wake usitekelezwe. Kwani kusafirishwa ni haramu kwa mujibu wa madhehebu sahihi yaliyochaguliwa na wengi. Wahakiki wameliweka hilo wazi.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 26/12/2019